![]() |
| Waumini wa Dini ya Kiislam wakishiriki ibada ya Eid |
![]() |
| Shekh wa Msikiti wa Nunge Ahmed Zuber akizungumza jambo wakati wa ibada ya Eid iliyofanyika katika uwanja wa jamhuri Jijini Dodoma |
![]() |
| Ibada ikiendelea [ PICHA ZOTE NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG] |
![]() |
| Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa Suleiman Jaffo katikati akishiriki ibada ya Eid jijini Dodoma |
Na John
Banda, Dodoma
Kamati ya
Sherehe za Kiislamu Jijini Dodoma imewataka waumini wa dini hiyo kuacha mizozo ikiwemo kutengeneza
vikundi vya mashindano badala yake wawe wamoja ili iwe rahisi kupata maendeleo
Akizungumza
katika Ibada ya Sala ya Eid – el – Fitr SHEKH wa msikiti wa Nunge Ahamed Zubery
amesema Damu haiwezi kufuta damu
“bila umoja
hatuwezi kuendelea hata kidogo tunayoyataka hatuwezi kuyapata tuondoleane mipaka
tuweni wamoja kwa kuwa vikundi visivyokuwa na maana vinazidi hebu tuondoleane mizozo
tusameheane kwa kuwa Damu haiwezi kufuta damu”, alisema
Aidha Sekh
Zubery amewataka Waumini hao kuacha mashindano na badala yake wajiingize katika
kutafuta Elimu ili kuondokana na manung’uniko ya kuonewa kila wakati.
Kwa upande
wake Ustaadh Omary akitoa mawadha katika ibada hiyo amesema imefika wakati
ambao kila muislam jijini Dodoma kuwachukua watoto yatima na wanaoishi katika
mazingira magumu ili kuishi nae njia ambayo itawasababishia Baraka
Tags
EID- EL - FITIR 2018






