BANDA MEDIA BLOG

No title


RAIS NA MWENYEKITI WA MAPINDUZI  ZANZIBAR DKT, HUSSEN ALLY MWINYI  MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA UBUNIFUFU YATAKAYOFANYIKA JIJI DODOMA MEI 16 MWAKA HUU
IMEANDALIWA NA BANDA BLOG


NA JOHN BANDA, DODOMA

RAIS na mwenyekiti wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt, Husein Ally Mwinyi natarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye  maadhimisho ya ubunifu na mashindano ya sayansi kitaifa

Akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dodoma Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (MAKISATU)2022 Prof Adolf Mkenda amesema kuwa Dkt, atafungua mashindano hayo mei 16 mwaka huu

Mkenda amesema maadhimisho hayo yanalenga pamoja na mambo mengine kuibua, kutambua na kuendeleza jitihada zinazofanywa na wabunifu wa kitanzania na kuhamasisha matumizi ya teknolojia na ubunifu wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii

Aidha amesema maadhimisho hayo ya wiki ya kitaifa ya ubunifu yanatoa fursa kwa wabunifu/wagunduzi kujitangaza na kujulikana kwa wawekezaji, watumiaji wa bidhaa zao na wadau wengine ndani nan je ya nchi

Ameongeza kuwa wiki ya ubunifu ni mkakati wa serikali way a awamu ya 6 wa kuhamsisha matumizi ya Sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo ya kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii

Amesema tayari maadhimisho hayo kimkoa yamesaanza katika mikoa 16 tangu aprl 27 ambapo kitaifa yatarajiwa kuanza mei 15 mwaka huu katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma na kwamba kilele kitakuwa mei 19 yakifungwa na makamu wa rais Philip Mipango

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG