Adeladius Makwega-DODOMA
Kanisa Katoliki limeipongeza
Hospitali ya Uhuru ya Wilayani Chamwino mkoani Dodoma iliyopo kandakando ya
Barabara inayokwenda Morogoro njia ya panda ya kuingia Chamwino Ikulu kwa
kuhudumia wagonjwa vizuri wanapofika hapo kutibiwa.
Hayo yamesemwa na Paroko wa
Kanisa la Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu Jimbo Kuu katoliki la Dodoma
Paul Mapalala katika matangazo mwishoni mwa misa ya kwanza ya dominika ya Mei
15, 2022 inayoanza saa 12 ya asubuhi ya kila jumapili.
“Nilikwenda hospitalini hapo
nikiwa mgonjwa sana, siku ya ijumaa na kweli madaktari, wauguzi na watumishi wa
hospitali hii walinipokea vizuri sana, wakanipatia vipimo, nikapatiwa dawa na
huku wakifika kunijulia hali hadi sasa nimepona kabisa.”
Moyo huu wa ukarimu kwa wagonjwa
ni moyo mwema sana nimeona nilivyotendewa mimi na wakitendewa wengine
hospitalini hapo kwa maana mgonjwa anapoumwa anahitaji faraja kubwa kwanza kwa
wahudumu wa afya na pili kwa jamii yake alipo, alisema.
“Ninawashukuru mno hata
waamini kadhaa waliojitokeza kuniona katika ugonjwa wangu hilo ni jambo jema na
hiyo ndiyo imani yetu.”
Alisisitiza Paroko Mapalala.
Hospitali ya Uhuru ni miongoni
mwa hospitali kubwa za serikali katika mkoa Dodoma ambayo ipo katika Wilaya ya
Chamwino kilomita kadhaa kutoka ilipo Ikulu ya Chamwino ambayo inato a huduma
mbalimbali za tiba.

