Afsa habari na mawasiliano wa TEA Eliafile Solla, akiwa pamoja na Mbunifu Frank Kisamo, wakiwaonyesha waandishi wa habari Mbolea hai inayotengenezwa kwa kutumia kinyesi cha wanyama na mabaki ya chakula ambapo mbunifu huyo aliibuni kwa kuwezeshwa na mfuko wa kuendeleza ujuzi (SDF)
Afsa habari na mawasiliano wa TEA Eliafile Solla akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma, kunakoonyeshwa kazi mbalimbali za ubunifu zinazofanywa na watanzania
Mjasiliamali Ester Shebe akimhudumia mteja Wine, iliyotengenezwa kwa malighafi ya Uyoga ambao pia anautumia kutengenezea keki,achali na biskuti, mwanadada huyo anawezeshwa na mfuko wa kuendeleza ujuzi (SDF)
NA JOHN BANDA, DODOMA
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA)
Imewashauri watanzania kuwa wabunifu ili kuleta maendeleo endelevu nchini hali
itakayowafanya kujiinua kiuchumi na kuondokana na umasikini
Pia, TEA imefanikiwa kuwawezesha
watanzania zaidi ya 32 elfu chini ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiriliamali yakiwemo ya
ubunifu katika sekta sita
Kauli hiyo imetolewa na Afisa habari na
Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Bi Eliafile Solla wakati
akizungumza na waandishi wa Habari katika Wiki ya Ubunifu Kitaifa 2022
(MAKISATU) Jijini Dodoma.
Aidha Bi Eliafile amesema Ubunifu ni
sehemu ya kila mtu ikiwa ataamua kujishughulisha bila kukata tamaa na kuongeza
ujuzi kwa kujiunga na mafunzo yanayotolewa na ruzuku ya mfuko wa kuendeleza ujuzi (SDF).
Eliafile ameongeza kuwa zaidi
ya watu elfu 32 nchini wamenufaika kwa kuwezeshwa kimafunzo na ubunifu wakiwezeshwa na mfuko wa kuendeleza ujuzi (SDF), ruzuku iliyojikita katika sekta sita za kipaumbele ambazo ni uchukuzi, nishati, ujenzi, utalii,na huduma za ukarimu, Teknojia ya habari TEHAMA pamoja kilimo biashara.
Maonyesho ya wiki ya wabunifu MAKISATU
mwaka huu yana kauli mbiu isemayo "Ubunifu kwa Maendeleo
endelevu".
Kwa upande wake mnufaika wa mafunzo ya mfuko wa kuendeleza ujuzi (SDF)' Malkia wa nguvu 2022 kilimo na Bishara Esther
Shebe, ambaye Aliacha kazi ya uuguzi tangu mwaka 2018 na kuamua kuwa mjasiriamali amesema
wanaishukuru serikali kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali kwani kupitia
mafunzo hayo wamejikwamua na umaskini.
Hata hivyo Esther amewashauri wanawake na vijana kujishughulisha kwa kufanya kazi zinazowaingizia kipato bila uoga ili waepukane na utegemezi.