KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake
na Makundi maalum Dkt. Zainabu Chaula,akizungumza wakati wa mkutano wa mafunzo
ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku
tano.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima
(hayupo pichani) wakati wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini
(SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima
(hayupo pichani) wakati wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini
(SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara
(NGOs) Neema Lugangira ,akizungumza wakati wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa
Machinga nchini (SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewahakikishia Wamachinga nchini kuwa katika mwaka wa fedha unaoanza mwezi
Julai Ofisi yake kupitia Tawala za mikoa na Serikali za mitaa itatoa Sh.
Milioni 10 kwa kila mkoa kuwezesha shughuli za machinga
.Rais Samia amesema hayo jijini Dodoma kwa njia ya simu mara baada ya kupiga simu moja kwa moja na kuzungumza na wamachinga waliohudhuria mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA).
“Nakushukuru Waziri kwa kuwapa Wamachinga Ofisi ambayo ni
jengo la Serikali,nimesikiliza risala
yao na nimefurahishwa,nakushukuru waziri kwa kuwapa ofisi atika majengo
ya serikali, nami niwahakikishie ushirikiano na mazingira mazuri ifikapo mwaka wa fedha unaoanza mwezi Julai
nitatoa milioni kumi kwa Kila mkoa kuwezesha shughuli zao,”amesema
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima,amempongeza Rais Samia
kwa uamzi huo na kueleza kuwa umeleta tumaini jipya kwa Machinga nchini.



