TANZANIA YAADHMISHA SIKU YA MTOTO WA KIKE
Dar Es Salaam, 11 Oktoba, 2022.
Tarehe 11 Oktoba
ya kila mwaka Tanzania hungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa
kuadhimisha Siku ya Kimataifa
ya Mtoto wa Kike ambapo lengo la maadhimisho ni kutoa fursa kwa wadau
wanaotekeleza afua za watoto hususani watoto wa kike kufanya tathmini ya
upatikanaji wa haki, ulinzi na maendeleo ya watoto kwa ujumla na kupendekeza
hatua stahiki katika kuboresha huduma hizo.
Vikundi hivyo
vimetoa mchango mkubwa katika kuhamasisha jamii kuachana na vitendo vya ukatili
dhidi ya watoto, kuchangia nguvukazi katika ujenzi wa vituo vya kijamii vya
malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na kuimarisha nidhamu ya wazazi
na watoto kwa kuendelea kutoa elimu hiyo katika ngazi ya jamii.
Katika nchi yetu
maadhimisho haya yatafanyika katika ngazi ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za
Mitaa na yatafanyika kulingana na mazingira ya Mkoa na Halmashauri husika. Ni
muhimu kwa kila Mkoa kufanya maadhimisho haya ili kuelimisha wananchi kuhusu
umuhimu wa kutoa haki kwa kuzingatia usawa wa kijinsia kwa watoto wote.
Wizara
itashirikiana na Mkoa wa Mara katika kilele cha maadhimisho haya
kitakachofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti. Aidha, Wizara
itashirikiana na Mkoa wa Manyara katika kufanya kampeni ya kutokomeza ukatili
dhidi ya watoto hususani ukeketaji katika Wilaya zote za Mkoa huo ambapo kilele
cha kampeni hizo itakuwa tarehe 12 Oktoba, 2022 katika Halmashauri ya Mji wa
Babati.
Mwisho,
natoa rai kwa wananchi wote kuhamasishana kuhusu Haki, Ulinzi, Ustawi na
Maendeleo ya Watoto hasa watoto wa kike ambao ndio wahanga wakubwa katika
familia na Jamii. Niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi katika Mikoa na
Halmashauri zetu kushiriki kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto wa
Kike.