MHE. KAIRUKI AZINDUA MKAKATI WA UTEKELEZAJI WA SERA YA WANYAMAPORI NA MPANGO WA USIMAMIZI WA TEMBO

Na Happiness Shayo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amezindua Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Wanyamapori 2023 – 2033 na Mpango wa usimamizi wa Tembo Tanzania 2033 – 2033, lengo ikiwa ni kukabiliana na changamoto mbalimbali za Uhifadhi wa Wanyamapori.
Uzinduzi huo umefanyika usiku wa Desemba 15, 2023 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Amesema uzinduzi wa mkakati huo, ni mwendelezo wa mikakati ya Serikali ya kulinda rasilimali za Wanyamapori ambapo Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka mazingira ya kisera, kuimarisha mfumo wa kisheria na udhibiti wa uhifadhi, ulinzi, usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za Wanyamapori.



