JOKATE AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA KANISA KATOLIKI KIGANGO CHA KIJIJI CHA TANGA MBINGA
*Awezesha upatikanaji wa zaidi ya Tsh Milioni 30.
*Awezesha upatikanaji wa Mifuko 18 ya Saruji
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu Jokate Mwegelo, ameongoza Harambee ya kuchangia mwendelezo wa ujenzi wa Kanisa Katoliki Kigango cha kijiji cha Tanga Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma.
Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 15 Disemba, 2023 aliposhiriki katika misa takatifu iliyosalishwa na Mhashamu Baba Askofu John. C. Ndimbo, Askofu Jimbo Katoliki Mbinga ya kutoa shukrani kama familia kwa nafasi ya kuaminiwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa katika nafasi ya Katibu Mkuu wa UWT Taifa.

