Uchaguzi DRC 2023: CENI kuanza kutoa matokea ya awali
Raia wa DRC pia walipiga kura kwenye nchi tano Canada, Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na Afrika kusini. / Picha: ReutersAkizungumza kwenye mojawapo ya
vituo vya redio DRC, afisa wa ngazi ya juu wa Tume ya Uchaguzi CENI, Didi
Manara alisema kuwa Tume ya Uchaguzi itaanza kuchapisha matokeo ya awali ya
uchaguzi wa rais siku ya Ijumaa.
Baadhi ya maeneo kama vile mji
mkuu wa Kinshasa, tayari yameanza kushuhudia matokeo yaliyochapishwa nje ya
vituo vya kupiga kura.
Wananchi wa DRC wamepiga kura
kuchagua rais, wabunge wa kitaifa na kikanda pamoja na madiwani wa mitaa.
Mnamo siku ya Alhamisi, Tume
Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, CENI, iliongeza muda wa
kupiga kura katika baadhi ya maeneo.
Rais wa sasa Felix Tshisekedi,
ambaye alichukua madaraka mwaka 2019, anawania kiti hicho kwa muhula mwengine
wa pili.
Wagombea 18 wa upinzani pia
wanawania urais nchini humo.
