BANDA MEDIA BLOG

No title

 

Uganda: Wanamgambo wa ADF waua 3 siku ya Krismasi

Kundi hilo hatari la wanamgambo la ADF, lina ushirikiano na kundi la Daesh / Picha: AFP

Kundi la ADF limeendeleza mashambulizi yake nchini Uganda na kusababisha vifo vya watu watatu katika kijiji cha mbali kilichoko Wilaya ya Kamwenge, wiki moja tu baada ya kuwaua watu 10 katika eneo hilo.

Kundi hilo hatari la wanamgambo la ADF, linaloshirikiana na kundi la Daesh limemchoma moto bibi mmoja na watoto wawili hadi kufa siku ya Krismasi magharibi wa Uganda.

Mkuu wa Wilaya ya Kamwenge, Isiah Byarugaba ameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa washambuliaji hao waliteketeza nyumba huku watu wakiwa ndani.

"Waasi wa ADF waliwaua watu watatu, mwanamke mzee na wajukuu wake wawili, waliowateketeza nyumbani kwao jana usiku," alisema.

Ameongeza kuwa jeshi na polisi walikuwa wakiwafuatilia washambuliaji hao.

"Tuko eneo hilo kutathmini hali kamili, na (sisi) tunahamasisha jamii ya eneo hilo dhidi ya mashambulio ya woga kama hayo ya magaidi wa ADF dhidi ya raia wasio na hatia."

Mnamo Disemba 19, waasi wa ADF waliwaua watu 10 katika kituo cha biashara eneo la Kamwenge, wilaya iliyo karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambayo ni ngome ya wanamgambo hao.

ADF wanashutumiwa kwa kuwaua maelfu ya raia DR Congo haswa katika miaka ya hivi karibuni na kutekeleza mashambulizi kwenye mpaka karibu na sehemu ya Uganda.

Ingawa Uganda na DR Congo walizindua operesheni za pamoja za kijeshi dhidi ya ADF mnamo Novemba 2021, lakini waasi hao wameendelea na mashambulio yao.

Mnamo Oktoba 2023, watalii wawili wa kigeni waliokuwa fungate na mwelekezi wao waliuawa wakiwa ziarani magharibi mwa Uganda kwenye mashambulizi yaliyodaiwa ni ya Daesh.

Polisi pia wamewalaumu ADF kwa vifo vya watu kadhaa, wengi wao wakiwa wanafunzi, wakati wa uvamizi katika shule moja Magharibi mwa Uganda mwezi Juni.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG