BANDA MEDIA BLOG

No title

 USAMBAZAJI WA MABANGO YA   ELIMU  TAHADHARI  YA MAGONJWA  YA MLIPUKO WAENDELEA HANANG



                                    Na. Elimu ya Afya kwa Umma.

Katika kujiweka tayari katika kukabiliana na Magonjwa ya Mlipuko hususan katika maeneo yaliyoathiriwa na Mvua ikiwemo Hanang, usambazaji wa mabango ya uelimishaji  umeendelea katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kituo cha Afya Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara.

Miongoni mwa jumbe zilizomo katika mabango hayo ni pamoja na mbinu za kujikinga na Magonjwa ya Kuhara na Kutapika ambazo ni kunywa maji yaliyochemshwa au kutibiwa na dawa ya Klorini, kutumia choo kwa usahihi kila wakati na kutupa kinyesi cha mtoto katika tundu la choo na pia kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni baada ya kutoka chooni,  kabla ya kula au kumlisha mtoto na baada ya kugusa maji ya mafuriko au tope.

Ikumbukwe kuwa msukumo wa elimu ya afya Hanang umeelekezwa kutokana  na asilimia kubwa ya vyanzo vya maji hasa mlima Katesh kuchafuliwa na maporomoko ya tope na magogo yaliyotokana na mvua kubwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG