BANDA MEDIA BLOG

No title

 

WASAMBAZAJI WA PEMBEJEO ZA KILIMO WALALAMA UPUNGUFU WA MBEGU SOKONI, SERIKALI YAWATAKA KUUNGANA NA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tehama Wizara ya Kilimo Rashid Likiligo, Akiongea jambo na waandishi wa habari kwenye mkutano huo

Peter Kazungu Mratibu wa Farm to Market alliance, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari
Natisile Mollel ambaye ni muuzaji wa pembejeo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara,



                                                  Sehemu ya washiriki wa mkutano huo

                                         PICHA YA PAMOJA

            .........................................................

                   NA JOHN BANDA, DODMA

KATIKA msimu wa Mvua za Masika zinazoendelea Kunyesha Nchini kote zimeleta Neema kwa Mkulima anaelima na kutarajia mavuno, lakini pia kwa wasambaza Pembejeo ambao kipindi hiki ndiyo hasa kipindi cha kuchuma fedha kutokana na wateja wa nyenzo hizo kuongezeka.

Pia  Wakulima huhitaji kupata pembejeo ili kufanya shughuli zao lakini zimebainika baadhi ya changamoto ambazo huenda zikaleta ugumu kwa wakulima, na moja wapo Ikiwa ni kupanda kwa gharama ya pembejeo kama v ile mbegu sokoni.

     Changamoto hizo zimethibitishwa DESEMBA 15,2023 jijini,Dodoma na Natisile Mollel ambaye ni muuzaji wa pembejeo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, alipoongea na  waandishi wa mbalimbali vyombo vya habari wakati wa mkutano wa wadau wa pembejeo za Kilimo ulioandaliwa na Farm to Market Alliance.

“uhitaji wa mbegu sokoni hasa kipindi hiki cha masika ambapo katika maeneo Mengi ya nchi mvua zinaendelea kunyesha, huku upungufua ukiwa ni mkubwa na kusababisha bei kupanda,

Naweza nikasema kuwa hata bei za mbegu zimeongezeka kwani tofauti na mwaka jana ambapo jumla tuliuza 1500 kwa kilo mbili lakini kipindi hiki tunauza 1800 kwa kipimo hichocho”, amesema

 Kwa Upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tehama Wizara ya Kilimo Rashid Likiligo  amewaasa wasambazaji wa pembejeo hapa nchini kufanya kazi na serikali ambayo ndiyo yenye watu, nguvu na sauti hasa kipindi hiki ambacho huduma ya kilimo inatolewa kwa M - KILIMO 

 Naye Peter Kazungu Mratibu wa Farm to Market alliance amesema mradi huo ambao una lengo la kuwafikia kila wakiulima wote kwa kuwarahisishia wasambazaji kufanya kazi zao kwa urahisi Kigijitali, ambapo kwa Tanzania Mradi huo unafanya Kazi kwa takribani Mikoa sita.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG