Air B n B Kenya zaagizwa kushikilia vitambulisho vya wateja kudhibiti uhalifu
Mamlaka ya udhibiti wa usalama
binafsi PSRA nchini Kenya imewaagiza wafanya biashara wa kukodi vyumba vya muda
Air BnB, kushikilia vitambulisho rasmi vya wateja wao wanapokodi vyumba n akuchukua
maelezo yote kuwahusu kw alengo la kuimarisha usalama.
Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Usalama Binafsi, Fazul Mahamed alisema maagizo hayo
yanalenga kudhibiti matukio ya ukosefu wa usalama katika taasisi hizo kufuatia
mfululizo wa mauaji ya kutisha tangu mwaka uanze.
Chini ya agizo hilo wamiliko
wa vyumba watatakiwa kurekodi muda wa kuingia au kutoka kwa kila mtu binafsi
pamoja na magari au pikipiki zinazoingia au kutoka kwenye vituo hivyo.
Vutambulisho na vyeti vingine vyovyote vitarejeshwa
kwa wateja punde wanapoondoka.
Taarifa hiyo inanukuu kifungu cha sheria cha 48,
ambacho kinampa mamlaka afisa usalama wa kibinafsi aliyepo kwenye eneo la
kuingilia eneo au mali yoyote kumtaka mtu kujitambulisha, kusajili muda wa
kuingia na kutoka kwa mtu huyo na kuhifadhi kwa muda hati za utambulisho wa mtu
huyo.
Usalama wa data za wateja
''Taasisi zote pia zitahitajika kudumisha daftari
la matukio ya usalama ili kurekodi matukio muhimu ya kila siku yanayohusiana na
usalama wa wakaazi ndani ya majengo na kuhakikisha CCTV na kamera za usalama
ziko katika hali ifaayo ya kufanya kazi,'' iliendelea kusema taarifa hiyo.
Hata hivyo Mamlaka hiyo ilitoa onyo kali kwa
wafanya biashara hao kutofuja au kutumia vibaya maelezo binafsi ya wateja wao.
''Mtoa huduma za usalama wa kibinafsi ambaye
anakiuka Kifungu cha 48 cha Sheria hiyo, hutumia hati/maelezo ya kitambulisho
yaliyotolewa na watu binafsi wakati wa kuingia kwa eneo au mali yoyote kwa
madhumuni mengine isipokuwa kwa ajili ya utambulisho, na/au kwa makusudi
kushindwa kutii agizo hili, anavunja sheria,'' Taarifa ilisema.
Kwa mujibu wa onyo hilo, watakaokiuka sheria hiyo
pamoja na kufutwa kwa leseni, atawajibika kwa adhabu iliyowekwa chini ya sheria
ya kulinda maelezo ya siri ya watu, au sheria nyingine yoyote ambayo ni kubwa
zaidi.
katika siku chache zilizopita, wanawake kadhaa
wamekutwa wameuawa katika vyumba vya BnB jijini Nairobi ambapo mmoja alikutwa
amechomwa kisu na mwingine, katika tukio iliyohusiana, alikutwa amekatwa katwa
viungo vyake kwa kinachoaminiwa huenda ilikuwa tambiko la kishirikina.
Washukiwa kadhaa wanazuiliwa kusaidia polisi na uchunguzi.

