BANDA MEDIA BLOG

BAADHI YA VYAMA VYA SIASA MKOANI DODOMA VYAIKACHA CHADEMA KUHUSU MAANDAMANO YA TAREHE 24.MWEZI HUU.

 

Mwenyekiti wa Chana cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma, Yohana Mussa akifafanua jambo wakati akitoa Tamko la Kuyakataa maandamano yaliyotangazwa na CHADEMA , Kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari jijini Dodoma leo .

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mkoa wa Dodoma, Lailath Mbuta akisistiza Jambo kwenye Mkutno huo na Waandishi wa Habari

          ...........................................                          

                                             NA JOHN BANDA, DODOMA

 WATANZANIA wameshauriwa kulipuuza Tangazo la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Freeman Mbowe la kuwataka Kushiriki  maandamano Aliyotangaza  kufanyika Januari 24 mwaka huu kwa lengo la kuishinikiza  Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau wa uchaguzi nchini. 

 Hivi karibuni chama cha CHADEMA kupitia mwenyekiti wake  Ffreeman Mbowe kilitangaza maandamano ya Amani Bila kikomo Nchi Nzima, hadi Pale Serikali Itakapofanyia kazi Maoni na Mapendekezo ya Wadau kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya na Chaguzi huru na Haki, ambapo alisema maandamano hayo yanatarajiwa kuanza siku ya Jumatano ya Tarehe 24 mwezi huu.

 Alisema Maoni ya wadau hao yalitolewa wakati  Muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani wa mwaka 2023, Muswada wa sheria ya tume ya taifa ya uchaguzi wa mwaka 2023, na Muswada wa Sheria ya malekebisho ya sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 2023, ilipotolewa maoni Bungeni jijini Dodoma hivi karibuni.

 Viongozi hao wa Baadhi ya vyama vya Siasa Mkoani Dodoma wameyasema hayo mbele ya waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari jijini humo, ambapo wamewataka wananchi na wanachama wote vyama vyao kuyapuuza maandamano hayo na kuendelea na kazi zao za ujenzi wa taifa kwa kuwa mchakato bado unaendelea Bungeni. 

 Akiongea kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma Yohana Mussa amesema, Maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliyoyaita ya Amani Ukweli ni kwamba hayana Baraka na Ndani yake hayatakuwa ya Amani. 

"Sisi kama Chama cha ACT Wazalendo na wenyeviti wenzangu tunaamini maoni yetu yatazingatiwa na wabunge kwa kuwa tumeiona nia njema ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake Katika jambo hili, " Amesema.

  "Kwanini Sisi Wenyeviti tusema Maandamano haya sio ya Amani?, ni  kwa Kuwa CHADEMA  kimeacha mchakato halali wa majadiliano na fulsa iliyotolewa na Rais,Samia ya Maridhiano Kisiasa na kujenga umoja wa kitaifa lakini cha kushangaza, MBOWE na watu wake wanataka kuwaingiza watu barabarani kufanya maandamano katika nyakati hizi ambazo taifa letu linahitaji utulivu mkubwa, " Amesema Mwenyekiti huyo

 Naye Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) Stephen Chitema  amewaka wabunge kuzingatia maoni yaliyotolewa kikao cha Bungeni,  kuhusu mabadiliko ya katiba kwani Jambo  hilo ni la muda mrefu na limekuwa likitumia fedha nyingi. 

 Kuhusu maandamano ya tarehe 24, amesema Freeman Mbowe ameitisha maandamano ya wafuasi wake na wananchi, wakati ambao wananchi wapo mashambani wakiendelea na kilimo, 

 "Kwa wito huu anataka wananchi watoke kwenye shughuri za kilimo waje mijini kuandamana hii sio sahihi, " Amesema

 Amesema Mbowe anaitisha maandamano katika jiji la kibiashara Dsm huku akitambua juhudi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kufungua frusa za uwekezaji na biashara katika jiji ilo.

 "Lengo hapa sio maandamano ya Amani ila ni uharibifu wa juhudi za Mhe. Rais Katika Kuifungua Nchi

 "Sisi Wenyeviti wa Vyama Vya Upinzani Tuliopo Makao Makuu ya Nchini Tunampongeza Rais DK. Samia Suluhu Hassan Kwa Uamuzi Wake wa Kupeleka Bungeni Marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambapo sasa, kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria chini ya mwenyekiti wake Joseph Mhagama imetoa fulsa kwa wadau mbalimbali kutoa maoni yao Hivyo CHADEMA wajue kila mtu atatoa maoni kwa wakati wake,

 Amesema kamati ya bunge ilitoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau KIASI cha kutosha ilifikia baadhi ya wadau walipewa nafasi Zaidi ya mara moja kutoa maoni yao wakiwamo hawa wanaitisha maandamano

 "Chama cha Chadema na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe  imekuwa ni tabia yao kuacha michakato halali na kukimbilia kwa wananchi kujilizaliza, Sisi wenyeviti Imara tunasema hatuungi mkono maandamano hayo na tunalaani kwa nguvu kubwa ukiukaji huu wa maridhiano ya kidemokrasia yalianzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, " Amesema 

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Mkoa wa Dodoma, Stephen Chitema akizungumza katika mkutano huo na Waandishi wa Habari

Mwenyekiti wa Chama cha AAFP  Davis Sembuche Mkoa wa Dodoma, akichangia jambo katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Meshack Masinga akiongea jambo katika mkutano huo

Mwenyekiti wa Chama cha Democrasia Makini Mkoa wa Dodoma, Baraka Machumu akizungumza jambo kwenye Mkuno huo.


Waandishi wa habari wakiufuatilia mkutano huo wa baadhi ya viongozi wa Vyama vya Siasi, uliofanyika jijini Dodoma leo Januari 18,2024

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG