Paul Nthenge Mackenzie alikamatwa Aprili mwaka jana baada ya miili kugundulika ndani ya msitu wa Shakahola karibu na Bahari ya Hindi, / Picha: AFP
...........................................................
Mahakama nchini
Kenya siku ya Alhamisi imemtia hatiani Paul Mackenzie na wenzake 94 kwa
kusababisha vifo vya watu zaidi ya 400.
Hata hivyo,
Mchengaji Mackenzie na wenzake walikana mashitaka hayo, yakiwemo kuchochea
'itikadi kali' kati ya wafuasi wake pamona na 'uhalifu wa kupangwa', kulingana
na stakabadhi za mahakama ya Mombasa.
Mackenzie
anadaiwa kuwachochea wafuasi wake kushinda njaa ili wamwone 'Yesu', tukio
lililoushangaza ulimwengu.
Kiongozi huyo
wa Good News International Church alikamatwa Aprili mwaka jana, baada ya miili
kugunduliwa katika msitu wa Shakahola uliopo Pwani ya Kenya, huku uchunguzi wa
maiti ukionyesha kuwa wengi wa waathirika hao wapatao 429 walipoteza maisha yao
kwa njaa, kufuatia maelekezo ya Mackenzie.
Waathirika
wengine, wengi wakiwa watoto walionekana na makovu shingoni na sehemu zingine
za mwili, ikiashiria kuwa walinyongwa au kupigwa vibaya na kusababisha vifo
vyao.
Ilimchukua muda
kwa Mackenzie kujua siku na hatma yake Mahakamani Mombasa, baada ya upande wa
mashtaka kuomba muda zaidi wa kuchunguza kesi hiyo.
Hata hivyo,
ilitishia kumwachia huru dereva wa zamani wa teksi, iwapo mashitaka dhidi yake
hayatowasilishwa ndani ya siku 14.
Kesi hiyo ya kushtua, iliyobatizwa 'mauaji ya msitu wa Shakahola', ilipelekea Serikali ya Kenya kutaka udhibiti mkubwa wa madhehebu ya dini mbalimbali nchini humo.
