KANISA LA KKKT LAWATAKA WAKRISTO KUTAFUTA AMANI KWA WATU WOTE
Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo Dayosisi ya Dodoma, Mch. Stanley Tabulu, akitoa Baraka za mwisho baada ya Ibada hiyo wengine na wachungaji wa kanisa hilo.
Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo Dayosisi ya Dodoma, Mch. Stanley Tabulu na Mchungaji Samwel Ngajilo wakishirikiana kutoa Meza ya Bwana kwa Bi. Mkunde Mwanga(90) kwenye ibada hiyo ya Mwaka mpya wa 2024, Kushoto ni Stella Mwanga ambaye ni mkwe wa Bibi huyo.
waumini wakipata ushirika (Meza ya Bwana)
Waumini wakisikiliza mahubiri kwenye ibada hiyo
ibada ikiendelea
Ibada ikiendelea
Ibada ikiendelea
Baadhi ya wanakwaya wa kwaya Kuu ya kanisa na KKKT Dodoma
Waumini wakifuatailia matukio kwenye ibada hiyo
Waumini wakifuatailia matukio kwenye ibada hiyo
Dc wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi Godwin Gondwe (DOUBLE G) ni mmoja kati ya waumini walioshiriki ibada hiyo leo Jan 1,2024
NA JOHN BANDA,
DODOMA,
BANDA MEDIA ONE.COM
KANISA la Kiinjili la Kirutheli Tanzania Dayosisi
ya Dodoma limewaasa wakristo wa kanisa hilo kote Nchini kutafuta kuwa na amani
kwa watu wote kwa kuwa Yesu wanayemtukuza alikuja kuleta Amani Duniani.
Wito huo umetolewa na Msaidizi wa Askofu wa kanisa
hilo Dayosisi ya Dodoma, Mch. Stanley Tabulu wakati alipokuwa akitoa salamu za
Mwaka mpya wa 2024, kwa wakristo.
Amesema Amani ikiwepo kuanzia ngazi ya Familia kwa
mtu mmoja mmoja na kwa taifa kwa ujumla, kitakachozaliwa ni Mahusiano mazuri
yatakayo sababisha Upendo na Furaha
katika jami, ambavyo vitazaa maendeleo.
“Wito wetu katika kanisa ni kwa wakristo kutafuta
kuwa na amani na watu wote kwani hata Yesu Mwana wa Mungu aliekuja Duniani
alikuja kuleta Amani.
Aidha amesema
Wajitahidi kuwapeleleka watoto Shule maana Urithi pekee kwao ni Elimu, “ hata
maandiko yanasema usimnyime mtoto Elimu kwani Elimu ndiyo Urithi pekee kwa mtoto