BANDA MEDIA BLOG

No title

 KANISA LISILO NA NGUVU ZA KIUCHUMI LIPIGWA NA NGUVU ZA GIZA NA KUPOTEA KABISA - DR. CHILONGANI

Askofu wa Kanisa la Angalikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dr. Dickisn Chilongani, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa George Malima mara baada ya Ibada hiyo

Canon Meshaki Sudayi akihubiri katika ibada hiyo, ambayo ujumbe ulikuwa ni kupewa jina jipya
                  Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa George Malima akiwa katika Ibada hiyo
                                                     w aumini wakiwa katika ibada hiyo
           Baadhi ya waimbaji wa kwaya maarufu ya Uvuke wakiimba katika ibada hiyo
Mke wa Askofu Pendo Chilongani akisalimiana na waumini wa kanisa la Angalikana baada ya Ibada
                                                 Ibada ya mwaka mpya ikiendelea
                                      Ibada ya Mwaka mpya wa 2024 ikiendelea

                     Waumini wa kanisa hilo wakifurahia jambo kwenye Ibada hiyo
                Mchungaji Makonde akitoa huduma ya Meza ya Bwana kwa washirika

         

Askofu Chilongani akisalimiana na Mmoja wa waumini wa Muda mrefu wa kanisa hilo.

            NA JOHN BANDA, DODOMA,

              BANDA MEDIA ONE.COM

               .......................................................

BAADA ya Kanisa anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika ( DCT) kukamilisha na kuzindua jengo la Kitega Uchumi la SAFINA lililopo Nje ya  kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, jijini Dodoma mwaka uliopita limewataka makasisi kuanzisha miradi katika makanisa  yao.

“mwaka uliopita tulikamilisha na kuzindua Jengo la Kitega uchumi la SAFINA, Mpango wa mwaka huu mpya wa 2024, ni kukamilisha Radio na Tv. Ili tufikishe utume wetu kwa njia ya kisasa zaidi, na makasisi wote waliyopo katika parishi za mjini waanzishe vitega uchumi vya kujenga fremu kwenye maeneo yao, wakishindwa baada ya mwaka mmoja nawaondoa mjini”,

Akiongea na BANDA MEDIA ONE.COM mara baada ya Ibada ya Mwaka  mpya wa 2024, Iliyofanyika katika kanisa kuu la Roho Mtakatifu jijini Dodoma, Askofu Dr. Dickison Chilongani amesema kanisa ili liweze kumudu kafanya huduma mbalimbali zikiwemo za Utume, kusaidia wahitaji, Afya Elimu na kujiendesha lazima liwe na nguvu za kiuchumi.

“sisi wakristo tunaangalia sana mambo ya kiroho tukitaka kuhubiri na kuomba zaidi lakini tumesahau Agizo la Yesu kwenye kitabu cha Mathayo Mtakatifu 18;19,20 la Kututaka tukahubiri injili kwa kila kiumbe na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wake, sasa utawezaje kuhubiri bila kuwa na fedha”, alisema na kuhoji

Amesema yeye anavyoamini ili kanisa liweze kutimiza utume wake Mambo ya Kiroho na Kiuchumi yanaenda pamoja.

 Aliongeza kuwa Kanisa ambalo haliwekezi kwenye Uchumi, litatikiswa na Milango ya kuzimu na nguvu za Giza zitalishinda na kuliangusha kabisa mwishowe litapotea kabisa na halitaonekana tena.

Kanisa litakalodumu ni lile tu ambalo litakuwa imara kiroho na kiuchumi ndilo litakalodumu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa George Malima aliehudhuria ibada hiyo ya kumshukuru Mungu kwa kamaliza na kuunza mwaka 2024, amesema kanisa linapokuwa na nguvu imara za Kiuchumi, wachungaji wake hawawezi kuombaomba

“kinachowafanya watumishi wengine kubaki wakiombaomba ni kutokana na makanisa kukosa nguvu za Kiuchumi, hiyo ni sababu kubwa pia ya kubuni njia za kuwatoza waumini wao ambao pia hawana kipato cha kutosha sadaka nyingi”, amesema

        

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG