YPDEA imemuomba Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kutengeneza Mazingira rafiki ya Kujiajili ikiwemo kwenye Kilimo ili kuwaepusha baadhi ya wanawake kujihusisha na Biashara za ngono wanazoangukia baada ya kukata tamaa kimaisha.
Mshauri wa Rais wa Taasisi ya YPDEA Vicent Malendaa Akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa taasisi hiyo mkoa wa Dodoma.

Wajumbe wa Taasisi ya Kiraia ya YPDEA mkoani Dodoma wakiwa katika kikao chao kilichofanyika jijini Humo.
Msahuri wa Rais wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya YPSEA Vicent Malendaa, Afisa Kilimo Taifa Neema Chiboni, Mratibu Idara ya Vijana na wanafunzi wa Vyuo vikuu na Sekondari Ashura Moshi, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dodoma Frank Tesha na viongozi wa Halmashauri za wilaya na manispaa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao hicho.
…………………………………………
NA JOHN BANDA, DODOMA
TAASISI ya Kiraia ya
YPDEA imemuomba Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kutengeneza Mazingira rafiki ya Kujiajili ikiwemo kwenye Kilimo ili
kuwaepusha baadhi ya wanawake
kujihusisha na Biashara za ngono wanazoangukia baada ya kukata tamaa kimaisha.
Pia kuisadia Serikali
kwa kuhamasisha amani kuanzia ngazi za mitaa, kata, mikoa hadi Taifa kwa
kufichua Waovu na maovu yaliyopo katika jamii
Mratibu wa Vijana na
Wanafunzi wa vyuo Vikuu na sekondari wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya YPDEA
inayojishughulisha na Vijana kwenye Maswala ya Amani, Uchumi na Maendeleo,
Ashura Moshi alipoongea na waandishi wa habari kando ya kikao cha taasisi hiyo
Kimkoa kilichofanyika jijini Dodoma.
“Tunamuomba Rais Samia
na Serikali yake waweke mazingira wezeshi kwa wanawake yatakayowawezesha
kujiajili katika miradi mbalimbali ikiwemo kuwatengea maeneo ya kilimo kwa kuwa
kila mmoja atakapojibidiisha kwa kazi,
Watu wakifanya kazi
zao katika mazingira ya kuvutia watajenga uchumi wao na hatimaye vitendo hatarishi
kama vya biashara hatarishi za ngono kwa baadhi ya wanawake, Madawa ya Kulevya
na vitendo vya ushoga kwa baadhi ya vijana wenzetu vitapungua kama siyo kwisha
kabisa”, amesema
Awali Mshauri wa Rais
wa Taasisi hiyo Vicent Malendaa, akiongea kwenye Kikao hicho amesema moja ya
Majukumu ya Taasisi hiyo ni pamoja na Kuwakusanya vijana pamoja na kuwatia moyo
wa kuendelea na maisha kwa kujishuhulisha bila kukata tama, huku YPDEA
ikiwatafutia na kuwanganisha na fursa mbalimbali za kiuchumi.
Aidha amesema katika
moja ya Tafiti zake alizowahi kufanya aligundua kuwa sababu kubwa ya kufanya
familia nyingi kuwa katika Mdororo wa Kiuchumi, pamoja na kukosa maendeleo ni
kutoaka na Baadhi ya wanandoa kuishi bila amani kunakosababishwa na kiburi cha
Fedha na kazi kwa Mwanamke Huku Mwanaume akikataa kuonewa, hivyo taasisi hiyo
itahakikisha inatoa Elimu ya Umuhimu wa Amani kwa ngazi zote.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Mkoa wa Dodoma, Frank Tesha amesema Vijana wengi wanapofeli kwenye mipango
yao ya kimaisha kupitia shughuli wanazokuwa wakifanya, wanajikuta wametumbukia katika mambo ya uvunjifu wa maadili
unaopelekea wengi wao kupoteza Dira nzima ya maisha ambapo YPDEA ipo kwa ajili
ya kuwashika mkono na kuwarejesha tena katika matumaini mapya.