Uzalishaji wa kahawa barani Afrika unapungua kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi. / Picha: Reuters
Viongozi wa Umoja wa Afrika katika mkutano wao kwa
kila mwaka tarehe 17 na 18 Februari mwaka huu walikubaliana kwa pamoja kuwa
kahawa iangaliwe kama zao la kimkati barani Afrika.
"Huu ni ushindi mkubwa kwa Uganda," Waziri
wa Kilimo Frank Tumwebaze amesema katika mtandao wa X.
Uganda ni kati ya wazalishaji wakubwa wa kahawa
barani Afrika.
Kulingana na Shirika la Kimataifa la Kahawa,
uzalishaji wa kahawa barani Afrika ulipungua kwa asilimia 7.2 kwa mwaka 2022/23
hadi magunia milioni 17.9, kutoka Magunia milioni 19.3 katika mwaka uliopita wa
kahawa.
Shirika hilo linasema hii ilifanyika huku sehemu ya
soko ya pato la dunia ikishuka kidogo hadi 10.6% kutoka 11.5%.
"Uganda ilikumbwa na upungufu wa uzalishaji
kutoka asilimia 6.8 katika mwaka wa kahawa 2022/23 hadi magunia milioni 5.6
kutoka milioni 6.0 mifuko katika mwaka wa kahawa 2021/22.
"Huo ulikuwa ni mwaka wa pili mfululizo wa
kushuka kwa uzalishaji, kupungua kwa sababu sawa na ilivyokuwa mwaka wa kahawa
2021/22 yaani kuendelea kwa ukame. Iliripotiwa mara ya kwanza mapema Februari
2022, ukame huu uliathiri maeneo mengi yanayolima kahawa," imesema.
Kwa jumla kuna nchi 25 Barani zinazo wekeza katika
uzalishaji wa kahawa.
Ethiopia inaongoza katika uzalishaji wa kahawa lakini
nayo pia imekumbwa na athari ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo imefanya
takriban familia za wakulima wadogo milioni 2.2 zinazojishughulisha na
uzalishaji wa kahawa zimepata mapato duni.
Ukame huu pia ulikumba nchi ya Kenya na kupunguza
uzalishaji yake.
Kenya ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa kahawa aina
ya Arabica barani Afrika, na pato lake lilipungua kwa asili mia 4.6% hadi
magunia milioni 0.73 mwaka wa kahawa 2022/23 kutoka magunia milioni 0.76.
Kwa kuiangalia kahawa kama zao la kimkakati
inamaanisha kuwa Umoja wa Afrika utaipa kipaombele uzalishaji wa kahawa, na
huenda ikaongeza uwekezaji wa kibara wa teknolojia ya kuongeza thamani ya
kahawa.
