Kuna uhamishaji wa teknolojia duni unaotumika kusaidia idadi kubwa ya uwezo wa sasa wa utengenezaji chanjo. / Picha : X- William Ruto
.......................................................................
Viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Addis Ababa
Ethiopia wameweka azimio la kujikimu kama bara katika utengenezaji wa chanjo
kufikia mwaka 2040.
Hii ni kutokana na somo kali wanaosema wlaijifunza
wakati wa janga la CVOID 19, ambapo Afrika ilionekana kubaguliwa katika utoaji
wa chanjo.
Rais wa Kenya WIlliam Ruto aliyeongoza kamati ya
viongozi juu ya chanjo, alisema wameafikiana kutafuta namna ya kujikimu ili
kuondoa utegemezi wa magharibi katika suala la kufa kupona kama hilo.
''Janga la Covid-19 lilifichua hali mbaya ya
utengenezaji wa dawa barani Afrika, pamoja na ile ya chanjo,'' alisema Rais
Ruto katika mtandao wake wa X. ''Tulikuwa bara la mwisho kupata chanjo za
Covid-19, na tuliteseka sana kutokana na 'utaifa wa chanjo','' aliongezea.
anga la Covid-19 lilifichua hali mbaya ya utengenezaji wa dawa barani Afrika, pamoja na ile ya chanjo/ Picha : X- Rais William Ruto
Tumejifunza na tumekoma
Rais Ruto, alielezea kuwa janga la COVID lilifichua
kile ambacho kilikuwepo kimefichwa miaka mingi, kuwa kila mmoja ana maslahi ya
watu wake kwanza kabla ya kuzingatia wengine, na Afrika inatakiwa kufuata
mkondo.
''Lakini hali hii itabadilika kuwa bora. AU imeazimia
kuwa ifikapo mwaka 2040, asilimia 60 ya chanjo zinazotumika barani Afrika
zitazalishwa nchini humo,'' aliendelea kusema Rais Ruto.
Tangazo hili linaendana na Ushirikiano wa
Utengenezaji Chanjo wa Kiafrika (PAVM) ulioundwa ili kuimarisha mfumo ikolojia
wa utengenezaji wa chanjo wa Kiafrika kufikia mwaka 2040.
Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya kudhibiti
magonjwa Afrika (ACDC), uwezo wa kutengeneza chanjo wa Kiafrika umejikita zaidi
kwenye mfumo wa kutengeneza, kujaza na kumaliza chanjo yote, huku kiwango
kikubwa cha uwezo wa ziada bado kikiwa katika awamu ya mipango.
Africa CDC inahofia kuwa iwapo mipango yote
itatekelezwa, uwezo wa kuunda, kujaza na kumaliza chanjo ungekuwa zaidi ya
maradufu ya makadirio ya mahitaji ya chanjo ya Kiafrika mwaka wa 2030. Katika
kiwango hicho cha uwezo, kuna hatari sio kila mradi wa utengenezaji ungekuwa
endelevu na wa kibiashara.
Hata hivyo wataalamu wanashauri kufanywa utafiti
zaidi kupata taswira halisi ya mapungufu na mahitaji katika mfumo ikolojia wa
utengenezaji wa chanjo ili kuhakikisha washikadau wote pania kusonga mbele na
miradi mipya na uwekezaji.
PAVM inalenga kuanzisha vituo vitano vya utafiti na
utengenezaji wa chanjo katika bara katika kipindi cha miaka 10-15 ijayo, na
kuongeza sehemu ya chanjo zinazozalishwa barani kwa ajili ya matumizi ya bara
hilo hadi 60%.
Ustawi wa mauzo ya chanjo barani
Tayari mataifa kadhaa ya Afrika yamewekeza katika
utengenezaji wa chanjo kupitia ufadhili wa kifedha na kimkakati kutoka kwa
taasisi ya chanjo barani Afrika MAV, ikiwemo Kenya, Morocco, Afrika Kusini,
Nigeria na Ghana.
Africa CDC imeelezea changa moto kubwa inayokabili
Afrika ni iutegemezi wa bara kwa uhamishaji wa teknolojia kutoka kwa
watengenezaji wa chanjo wasio Waafrika.
Lakini kuna uhamishaji wa teknolojia duni unaotumika
kusaidia idadi kubwa ya uwezo wa sasa na uliopangwa wa utengenezaji wa chanjo.
Utafiti pia ulihitimisha kuwa baadhi ya watengenezaji
chanjo wa Kiafrika tayari wana uwezo mkubwa wa kifedha (njia za kupata ufadhili
wa vifaa na shughuli zinazohitajika kuzalisha chanjo) lakini wanahitaji kukuza
zaidi uwezo wao wa kibiashara.
Miongoni mwa mapendekezo kuhusu njia ambazo
watengenezaji chanjo wa Kiafrika wanaweza kuboresha uwezekano wao wa kufaulu ni
pamoja na kuzingatia chanjo ambazo zina uwezo mkubwa wa soko na kuimarisha
mipango ya biashara.

