BANDA MEDIA BLOG

JUMAMOSI SIO MCHEZO WA KITOTO NI MECHI YA KIKUBWA-ALLY KAMWE

 

“Kilichosaidia CR Belouizdad ni wingi wa mashabiki wao, ukweli ni kwamba sisi sio wanyonge kimsingi hatuwezi kufanikiwa bila uwepo wa mashabiki wetu ambao kwa dakika zote tuwe na sapoti kubwa, kuanzia dakika ya kwanza mpaka dakika ya mwisho, tusishangilie matokeo tunapaswa kushangilia kila dakika kuhakikisha mwarabu anapagawa.”

“Jumamosi sio mchezo wa kitoto, ni mechi ya kikubwa kweli. Benchi la ufundi kimsingi limejiandaa vya kutosha kwa upande wa mashabiki tunapaswa kufika na hasira ya kweli kila anayeamini analo jambo ambalo linaweza kusaidia timu yako kushinda basi lifanye,ruksa popote ulipo usimuogope mtu wewe fanya. Hakuna masihara mchezo ujao, tukitoka sare basi ujue tumeisha” Ally Kamwe Meneja Habari na Mawasiliano Young Africans SC

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG