BANDA MEDIA BLOG

BALOZI KASIKE AKUTANA NA BALOZI WA MAWASILIANO WA ESWATINI

 

Katika kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Ufalme wa Eswatini, kwenye Sekta ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Eswatini na Madagascar alikutana na Mhe. Chief Ndlaluhlaza Ndwandwe, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Ufalme wa Eswatini, tarehe 28 Machi 2024, mjini Mbabane.

Wakati wa Mkutano huo, Viongozi hao wawili walikubaliana kuendelea kushirikiana kwenye sekta ya ujenzi wa Miundombinu kwa kubadilishana utaalamu na uzoefu sambamba na kuangalia uwezekano wa kushirikiana kwenye Sekta ya Usafiri wa Anga hasa baada ya nchi hizi mbili kufanikiwa kufufua Mashirika yao ya Ndege.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania – Maputo

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG