|
Naibu Katibu Mkuu wa Wizaraya Fedha, Bi Amina Khamis Shaaban, akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati, ambapo Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) aliongoza mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, kutokea Jengo la Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma. Makamu wa Rais wa Benki ya
Dunia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwaka, akitoa
mada wakati wa mkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika
Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati, ambapo Waziri wa Fedha Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) aliongoza mkutano huo uliofanyika kwa njia ya
mtandao, kutokea Jengo la Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma. |
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)
Na. Peter Haule, WF,
Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameongoza mkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la
Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati uliolenga
kujadili namna mashirika ya fedha ya kimataifa yanavyoweza kuongeza fedha kwa
ajili ya kuzisaidia nchi za kipato cha kati ili ziweze kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo katika nchi zao itakayochochea ukuaji wa uchumi na
maendeleo ya jamii.
Akifungua mkutano huo
uliofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mhe.
Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa Dunia inakabiliwa na migogoro mingi na
changamoto za maendeleo ya kiuchumi ambazo zinasababisha kutofikiwa kikamilifu
kwa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Alisema kuwa kupungua kwa
nafasi ya kifedha katika kushughulikia migogoro hiyo kunadhoofisha uwezo wa
Serikali za nchi hizo kufadhili programu za kijamii, kuharakisha ufufuaji wa
Uchumi na pia kuongeza madeni katika nchi hizo.
“Mizozo inayoendelea nchini
Urusi na Ukraine, Mashariki ya Kati na baadhi ya nchi nyingine za Afrika
imechochea kupanda kwa bei ya vyakula na kuwasukuma mamilioni ya watu kwenye
uhaba wa chakula”, alisema Dkt. Nchemba.
Aidha Dkt. Nchemba
aliishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake wa kuzijengea uwezo taasisi katika
kuyafikia maendeleo endelevu lakini pia kufufua uchumi kutokana na changamoto
mbalimbali zinazotokea Duniani.
Vilevile alisema kuwa
kukabiliana na changamoto zinazoikumba dunia sio kazi rahisi kwa nchi moja,
hivyo ameomba kuwa na nguvu ya pamoja katika Kanda na Bara la Afrika katika
kutafuta utatuzi wa changamoto hizo.
Dkt. Nchemba ameishukuru
Benki ya Dunia kwa kummwamini kuongoza kikao hicho kikubwa lakini pia
amewashukuru viongozi mbalimbali waliotoa mada ambazo zimewafunbua macho kwa
kuona fursa zilizopo katika kukuza una kuwezesha biashara na pia kuwa na
majadiliano mazuri wakati wa mikutano ijayo ya majira ya kipupwe ya Benki ya
Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) itakayofanyika mwezi Aprili, 2024
jijini Washington D.C nchini Marekani.
Kwa upande wake Makamu wa
Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika,
Bi. Victoria Kwaka, alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ilitoa misaada
na mikopo nafuu yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni tatu kwa nchi za Kanda
ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Alisema kuwa mwaka wa fedha
uliopita Benki ya Dunia kupitia Mfuko wa IDA ilitoa dola bilioni 2.4 na kwamba
kiwango cha misaada na mikopo hiyo imeendelea kuongezeka na miongoni mwa nchi
zilizonufaika na mpango huo ni Tanzania, Kenya na Eswatini.
Aidha, Bi. Kwakwa amevitaja
vipaumbele vya Benki hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha nchi zitapata umeme wa
uhakika, kuwa na maendeleo ya kidigitali, upatikanaji wa ajira, mapinduzi ya
kiuchumi, kujenga uwezo kwa rasilimali watu na masuala ya elimu.
Baadhi ya Viongozi
walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia
anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa,
Makamu wa Rais wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Kanda ya Afrika, Bw.
Sergio Pimenta, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, Bi. Anshula Kant,
Mawaziri wa fedha na Mipango (Magavana) na wajumbe wengine.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
