Kifupi ndo 'BIG MECHI' kwa sasa Afrika nzima. Kutokana na namna inavyoongolewa, kusubiriwa, kujadiliwa na hata timu husika zinavyojiandaa.
Mamelodi Wapo Bongo wanasubiri muda ili kuingia timu uwanjani. Wakati Al Ahly ambao walikipiga jana na Simba, wametanguliaza mguu mmoja hatua inayofuataya nusu fainali, kutokana na ushindi wa 1.0 walioupata kwa mkapa.
Kwa maana hiyo Mamelodi wamepata hofu. Hawana uhakika na matokeo yao kwa Mkapa. kutokana na Ugumu wa timu ya Yanga waliionyesha siku za hivi karibuni ikiwemo timu hiyo kucheza fainali za shirikisha Africa, ikichagizwa na asilimia kubwa ya wachezaji wake waliokuwa kwenye timu zao za taifa kuuwahi mchezo huo utakaopigwa leo saa 3 usiku
Kulifanyika mechi kubwa kama Simba na Al Ahly uzinduzi wa African Football League. Simba na Wydad robo fainali ya Klabu Bingwa msimu wa jana. Na hata Yanga na Belouzidad kupambania kuingia robo.
ukubwa wa Yanga umevifanya vyombo vya habari na wachambuzi wakubwa africa kuichambua mechiyao kwani hata Mamelodi si wakubeza..
Lakini mechi ya Yanga na Mamelodi itakuwa kubwa kuliko. Haijawahi kutokea mechi kubwa ya klabu ya kiwango kama hiki. Hii ni zaidi ya mechi. Zaidi ya tukio na zaidi ya msisimko.
inaonekana Mamelodi wametepeta kabla ya muda kuwadia.
