BANDA MEDIA BLOG

ZANZIBAR ILIJIUNGA NA OIC KUTOKANA NA UMASIKINI - SAFARI YA MZEE WA RUKHSA

 


IKIWA Leo ni siku ya Tano ya Maombolezo ya Mzee Ruksa aliyefariki February 29, mwaka huu majira  ya saa 11 jioni, ambapo mwili wake ulizikwa machi 2, nyumbani kwake Manga Pwani Zanzibar

Tuendelee kukipitia Kitabu cha Safari yake yapo mengi ya kujifunza ...!!

Mzee wa Rukhsa anasema pia kuna suala la OIC ambalo kwa sababu ya umaskini na kuendekeza misaada Zanzibar iliamua kujiunga na Umoja wa nchi za Kiislam na ilipelekea mjadala mkali Bungeni na  hatimaye Zanzibar ilijitoa. 

Anasema OIC ilipelekea hoja ya Tanganyika ya G55 ambapo Wabunge walitaka Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano hata hivyo baada ya hoja kupita. Mwalimu hakukubali na kiliitishwa kikao cha NEC Augost 24 1994 na kuhitimisha jambo hilo. 

Mwalimu kipindi hicho aliandika kitabu cha  Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania, ambapo aliushambulia Utawala wa Mzee Rukhsa na kuwaponda Malecela na Kolimba kwa kumyumbisha Rais. Kama si Mwalimu Nyerere huenda Muungano usingekuwa kama ulivyo leo.

 Hata hivyo Mzee Rukhsa anasema kuwa Mwalimu hakuwa akimpinga sana na kama asingetaka mabadiliko aliyokuwa akifanya angeweza kuyazuia. Anasema alijitahidi kwa uwezo wake kutokujibizana naye.

Mzee Rukhsa anakiri kuwa kuna matatizo na madhaifu yaliyojitokeza wakati wa sera zake za Rukhsa lakini anatoa mfano wa kufungua madirisha ili kupata hewa safi lakini hapo hapo na inzi na mbu nao wanaingia ndani. 

Mzee Rukhsa anasema tabia yake ya upole na usikivu ilimletea shida ikiwa ni pamoja na migomo ya Wanafunzi, migomo ya Wafanyakazi nk. na ametoa kisa cha Walimu waliokuwa na madai ya posho na mishahara ambayo iwapo yangetekelezwa yalikuwa yanazidi bajeti ya serikali ya miaka mitatu. Walipokataliwa waligoma na baadae walilazimika kurudi kazini.  

Anasema Wafanyakazi walianza naye vizuri lakini wakamaliza vibaya . Kulikuwa na migomo na kumnunia, mfano kwenye Mei Mosi ya 1994 hawakumwalika na badala yake wakamwalika Mwalimu  ambaye alikataa , lakini 1995 ilipofanyika  huko Mbeya alikubali. Pia Wanafunzi wa Chuo Kikuu waligoma hali iliyosababisha Chuo kufungwa na  baadhi ya Wanafunzi kufukuzwa. 

Endelea Kufuatilia BANDA MEDIA ONE.COM karika hatua inayofuata ....!!

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG