BANDA MEDIA BLOG

ALINISINGIZIA NIMEMBAKA

 

Jina langu ni KANDAKUWAWI kutokea Kigamboni, Dar es Salaam nchini Tanzania, nafanya kazi ya kupiga picha, ni kazi ambayo niliipenda tangu nikiwa mdogo, nashukuru nimeweza kufungua na studio yangu.

Changamoto kubwa katika kazi yetu ni kuwa kila anayekuja kupiga picha huwa kuna namna anaiwaza vile itatoka kichwani mwake kutokana na matakwa yao, sasa picha ikija tofauti inakuwa tatizo.

Kuna safari alikuja Dada mmoja kupiga passport size, baada ya kupiga alionyesha kuridhika nayo, ila tulivyoprint, ikawa tofauti na yeye alivyotaka.

Akaniomba nirudie kwa gharama ile ile, nilikataa maana mimi ningepata hasara sababu natumia wino kuprint na karatasi zake, hivyo kama anataka nirudie basi alitakiwa aniongezee hata fedha kidogo.

Nilivyokaa ilikuwa shida, alianza kunifokea na ukaibuka mgomvi kiasi kwamba alivunja camera yangu ambayo bei yake ni zaidi ya Sh5 milioni, ule ugomvi ulivuta watu wengi mpaka tukafikishana polisi.

Kufika polisi yule dada alidai nilitaka kumbaka ndani ya ofisi yangu na ndio sababu ya kuvunja camera yangu ili kujitetea, nilikana madai hayo na mvutano ukawa mkubwa sana.

Ilibidi ile kesi iende mahakamani na yule dada ndiye alifungua kesi ya ubakaji, kesi ile ilinipelekesha sana hadi kuniyumbisha kiuchumi kwa sababu ofisi ilinibidi nifunge kwa sababu ile camera aliyovunja ndio ilikuwa tegemeo kubwa sana.

Nilikonda ghafla kutokana na msongo wa mawazo, nilikuwa nawaza kama dada akishinda kesi ina maana nitafungwa, vipi kuhusu camera yangu ambayo aliivunja.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG