Katibu mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla akizindua Mfumo wa Utamburisho wa Mkaazi kwa njia ya Kijitali.
....................................................................
NA JOHN BANDA, DODOMA
KATIBU mkuu Wizara ya
Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla amezindua mfumo wa Anwani za Makazi utakaowawezesha
wananchi kupata barua za utamburisho kupitia simu zao za mikononi.
Katika Uzinduzi huo
uliofanyika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma , Aprili 16,2024 umeambatana na uagawaji wa Kompyuta
na Vishikwambi vitakavyotumiwa na watendaji wa kata na mitaa kwa baadhi ya
halmashauri hapa nchini kwa ajili ya majaribio ya miazi mitatu huku serikali ikiahidi kugawa vitendea kazi hivyo kwenye
kata zote 4,066 hapa nchini baada ya majaribio hayo
Akiongea Katika uzinduzi
huo Katibu Mkuu huyo amesema kuanzisha mfumo wa anuani za makazi ni utekelezaji
wa Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003; makubaliano ya Kikanda kupitia Umoja
wa Posta Afrika yaani Pan Africa Postal Union -PAPU; makubaliano ya Kimataifa
kupitia Umoja wa Posta Duniani yaani Universal Postal Union - UPU; na Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya miaka mitano, 2020 – 2025.
Amesema Kwa lugha rahisi, NAPA ni daftari la
kidijitali la ukazi ambalo linawezesha Serikali Kuu, Serikali za Mtaa/kata au
Shehia pamoja na mambo mengine kujua Idadi wa Watu walio kwenye eneo husika
hivyo urahisi wa kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia
uhalisia wa watu na huduma zilizopo katika eneo husika.
Ametabaisha kuwa mfumo huo utamuwezesha Mwananchi
kuweza kuomba anwani kijiditali. Aidha, mwananchi anaweza kuomba kuhamisha
anwani yake anayoishi kutoka sehemu moja kwenye nyingine kupitia simu ya
mkononi bila hitaji la kwenda Serikali za Mtaa huku ukiwawezesha Watendaji wa
mitaa/shehia/vijiji kushughulikia maombi ya wananchi kwenye mfumo wa NAPA kwa
kutumia simu au vishwambi.
Ameongeza
kuwa Wizara itahakikisha kuwa vishikwambi vinavyogawiwa vinakuwa na intaneti
hivyo watendaji hawataingia gharama za ununuzi wa Bando kwa muda wote wa
kipindi cha majaribio ili waweze
kumhudumia mwanananchi bila kikwazo chochote cha kimfumo.
“Majaribio
haya yatakuwa ya muda wa Miezi Mitatu na baada ya hapo Wizara itafanya tathmini
na kuboresha kulingana na matokeo ya tathmini husika” amesema
Aidha
amesema Baada ya hapo utafanyika
uzinduzi rasmi wa Mfumo ili uweze kutumika nchi nzima. Hatua hii itakwenda sambamba na kuhakikisha
Watendaji kwenye Kata zote 4,066 wanapata vishwambi kuwawezesha kuwahudumia
wananchi kupitia mfumo huu wakiwa mahali popote nchini.
Kwa upande wake Katibu
mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI ameziagiza Halmashauri zote ambazo zoezi la
majaribio limefanyika na Halmashauri ambazo majaribio yataendelea kufanyika
kuhakikisha zinasimamia vyema zoezi hili
kwa kushirikiana na wataalam.
Pia akaagiza kupatiwa
taarifa ya utekelezaji kila mwezi. Aidha, Halmashauri zote ambazo zoezi la
uhakiki wa taarifa za Anwani za Makazi limefanyika na zenyewe zianze kuwataka
wananchi kutumia Anwani za Makazi pindi wanapofika katika Taasisi mbalimbali
kupatiwa huduma, Hatua ambayo amesema itatusaidia kutambua vyema watu wanaohudumiwa
na hivyo kuongeza ufanisi katika masuala ya ufuatiliaji na tathmini mbalimbali
katika huduma.
Awali Waatalam wa
Mawasiliano wa Wizara ya Habari na mawasiliano walionyesha wasilisho lililoonyesha
ugumu ambao wananchi walikuwa wakiupata pindi walipohitaji Barua za utamburisho
wa mkaazi kwenye ofisi za watendaji ambapo walichelewa kupata huduma husika
kutokana na ukosefu wa vitendea kazi, uhaba wa miundombinu na umbali.
“Barua kwenye ofisi za
watendaji ilikuwa kama Donda ndugu lisilotibika kwa wananchi hali
iliyowasababishia kukosa huduma za msingi kwa wakati, ndiyo maana serikali
imekuja na mfumo wa anwani za makazi ambao ni mwarobaini ….”, amesema
(Picha zote na John Banda wa BANDA MEDIA ONE.COM)