...............................................................................................
NA JOHN BANDA, DODOMA
JESHI la Polisi nchini limeanzisha madawati ya Jinsia na Watoto 420
ili kukabiliana na matukio ya ukatili wa
kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto katika jamii.
Hayo yamebainishwa jijini
hapa leo Aprili 15,2024 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini Hamad Masaun
wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo
katika kipindi cha miaka 60 ya muungano.
Amesema kutokana na
kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto, serikali
ilianzisha dawati maalumu la kushughulikia matukio hayo ili kuwalinda watoto
kuishi katika mazingira salama na hatimaye kutimiza ndoto zao.
“Uanzishwaji wa madawati ya
Jinsia na watoto umesaidia kuandaa askari wenye mafunzo maalum ya kutoa elimu
juu ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya Watoto kwa makundi yote katika
jamii.
Ameongeza kuwa Kupitia
Madawati hayo huduma bora ya namna ya kuwahudumia waathirika wa vitendo vya
ukatili wa kijinsia imewezeshwa.
Aidha Waziri Masauni amewaonya
wanaotumia Mitandao ya kijamii kuwakashfu na kuwatuna Viongozi wa serikali Pamoja
na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba Sheria zipo na hazijalala.
“wanaotukana na kuwakashfu viongozi
kupitia mitandao ya kijamii Serikali inawafuatilia na hakuna atakayepona hata
kama kwa sasa bado hajakamatwa lakini anafuatiliwa, wale ambao wanayasapoti
matusi na kashfa hizo mitandaoni waangalie isije ikawa wao ndio rahisi kupatika”,
amesema na kuongeza
Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano yataadhimishwa Aprili 26, mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es laam.