*KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA CCM WILAYA YA DODOMA MJINI,BAHI NA KONDOA*
*🌍 DODOMA MJINI*
OFISI YA CCM DODOMA MJINI
*( OFISI YA MWENYEKITI)*
*🗓️ 14 /04 /2024*
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma mjini *Ndugu. CHARLES MAMBA* Amekutana na Wenyeviti wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya *BAHI* na Wilaya ya *KONDOA*,Lengo likiwa ni kupeana uzoefu na kutathimini hali ya kisiasa katika Wilaya zao ndani ya mkoa wa Dodoma katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ujao....
Wenyeviti Hawa wa Dodoma mjini,Kondoa na Bahi pia wamepata nafasi ya kuaminiwa na umoja wa Wenyeviti wote wa Ccm Wilaya zote nchini kuanza mipango ya maandalizi ya mkutano wa pamoja wa Wenyeviti wote wa Ccm Wilaya zote nchini, Lengo ni kupanga mikakati ya namna ya kuhakikisha chama cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa ujao wa 2024 na uchaguzi MKUU wa 2025....
Mkutano huo wa Wenyeviti wote unategemewa kufanyika hivi karibuni katika mkoa wa Dodoma Wilaya ya Dodoma mjini...
*TUSHIRIKI UCHAGUZI KWA UADILIFU NA KAZI IENDELEE*
*Dodoma mjini tuko tayari*
*Tutashinda kwa kishindo*
©2024
*Imetolewa na katibu wa Siasa na Uenezi ccm Wilaya ya Dodoma mjini*
WENYEVITI WA CCM WA WILAYA TATU ZA MKOA HUO WAKUTANA KUJINOA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
byJohn Banda
-
0


