Takriban watu saba wameuawa katika machafuko katika
jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, maafisa
wa eneo hilo walisema siku ya Jumamosi, baada ya watu kufanya maandamano
kupinga mashambulizi makali yanayofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa
Daesh.
Kwa mujibu wa vyombo vya usalama, kundi la waasi la
Allied Democratic Forces (ADF) lenye mfungamano na DAESH, wanadaiwa kuwaua
zaidi ya watu 40 katika shambulio katika kijiji cha Mayikengo wiki hii na zaidi
ya 80 katika mashambulizi dhidi ya vijiji vingine vya jimbo hilo wiki
iliyopita.
Ukosefu wa usalama umechochea ghadhabu kwa umma, na
kusababisha kuuawa kwa askari wawili na dereva wao katika eneo la Lubero na
umati wa watu ambao walichoma gari lao usiku wa kuamkia Ijumaa, afisa wa eneo
hilo Julio Mabanga aliiambia Reuters.
''Siku ya Jumamosi, mapigano zaidi katika eneo hilo
kati ya vikosi vya usalama na wakazi wa eneo hilo yalisababisha vifo vya watu
wengine watatu: raia, mwanajeshi, na wakala wa idara ya upelelezi ya taifa ya
ANR,'' Mabanga alisema.
Kwengineko katika mji wa Butembo, mamia ya vijana waliingia
barabarani wakiwa na vijiti, wakiimba nyimbo za kukemea ukosefu wa usalama
ulioenea.
''Meya wa Butembo, Mowa Baeki Telly alithibitisha
kuwa raia mmoja aliuawa wakati wa mapigano kati ya vikosi vya usalama na
waandamanaji mjini humo.
Wapiganaji waasi wa ADF wanaaminiwa kutokea nchi
jirani ya Uganda, lakini sasa wamekita kambi katika eneo lenye utajiri wa
madini Mashariki mwa Congo.
Baadhi ya viongozi wa magharibi kutoka nchi tajiri
duniani waliokutana Italia mwishonbi mwa wiki, walizungumzia migogoro
inayokumba ma eneo ya Sudan na DRC hasa kutokana na mashambulio yamakundi ya
waasi kama haya.
