BANDA MEDIA BLOG

JAJI ALIYEPIGWA RISASI MAHAKAMANI APOTEZA MAISHA


 Hakimu mkuu wa Mahakama ya Makadara nchini Kenya Monica Kivuti amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na afisa wa polisi alipokuwa akitekeleza majukumu yake, tukio ambalo lilitokea Alhamisi ya Juni 13 


Kivuti alipigwa risasi na Inspekta Mkuu Samson Kipchirchir, ambaye alikuwa anapinga uamuzi wa hakimu huyo wa kufuta dhamana ya mkewe na kumnyima dhamana ya pesa taslimu.

Jaji mkuu wa nchi Martha K Koome ameandika kwenye mtandao wa X kwamba Hakimu Mkuu wa Makadara Monica Kivuti "ameshindwa katika vita" dhidi ya "majeraha yake makubwa". hivyo kupoteza maisha

Polisi huyo aliyetambulika kwa jina la Samson Kipchirchir Kipruto aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wengine kufuatia shambulizi hilo

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG