BANDA MEDIA BLOG

ITEKELEJI MRADI WA EACOP UNAENDELEA -DKT. NCHEMBA


Akisoma Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Bungeni-Dodoma, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki ( EACOP), Serikali kupitia TPDC inamiliki asilimia 15 ya hisa ambapo hadi mwezi Mei 2024, Serikali imelipa Dola za Marekani milioni 307.3 sawa na asimilia 99.8 ya kiasi kinachotakiwa kulipwa cha Dola za Marekani milioni 308.

 Amesema kazi mbalimbali zinaendelea kutekelezwa ambapo shehena za mabomba ya mradi yenye jumla ya urefu wa kilomita 600 zimewasili nchini na mradi unatarajia kuendelea kupokea shehena ya mabomba yenye jumla ya 

urefu wa kilomita 100 kila mwezi kwa miezi 11 ijayo.

Ameongeza kuwa, kazi ya kulaza mabomba inatarajiwa kuanza mwezi Agosti 2024 na mradi kukamilika Desemba 2025.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG