BANDA MEDIA BLOG

MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE (JNHPP) WAFIKIA ASILIMIA 97.43


 *MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE (JNHPP) WAFIKIA ASILIMIA 97.43*

Akisoma Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Bungeni-Dodoma, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokea Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha jumla ya MW 2,115 ukiwa na takribani asilimia 37 ambapo hadi Aprili 2024 utekelezaji ulikuwa umefikia asilimia 97.43.

Amesema mradi huo umeanza uzalishaji umeme kupitia mtambo namba tisa (9) unaoingiza katika Gridi ya Taifa jumla ya MW 235 na hivyo, kuimarisha upatikanaji wa umeme ambapo hadi kufikia hatua hii jumla ya shilingi trilioni 6.01 zimetumika. 

Amesema kwa sasa kazi inaendelea ili kukamilisha ufungaji wa mitambo saba (7) yenye uwezo wa kuzalisha MW 235 kila mmoja. 

Aidha, Serikali imekamilisha Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Rusumo kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera ambapo mradi huu unahusisha nchi tatu (3) za Tanzania, Burundi na Rwanda ambao unachangia MW 26.7 katika Gridi ya Taifa.

 Amesema Serikali pia imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa MW 150 kwa kutumia nguvu ya jua katika eneo la Kishapu mkoani Shinyanga. Vilevile, Serikali inaendelea na ujenzi na ukarabati wa njia za kusafirisha na kusambaza umeme ambazo zinaunganisha maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG