NA JOHN BANDA, DODOMA
KUELEKEA uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa
kufanyika Mwezi Octoba mwaka huu na Ule Mkuu utakaofanyika Mwakani Waumini wa Dini
ya Kiislam wametakiwa kuiombea Serikali Inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu
Hassani iweze Kunyooka
Wito huo Umetolewa leo June 17,2024 na Shekhe Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Alhaji Mustafa Shaban
wakati alipokuwa akitoa Mawaidha kwa Waumini Hao waliokuwa kwenye Ibada ya Eid
Ul Adha iliyofanyika katika msikiti wa Gadafi.
Shekhe amesema wakati nchi inajiandaa kuelekea kwenye
uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Mwezi wa 10 mwaka huu na ule wa
Mwakani nivizuri kila Muumini Kuiombea Nchi na Serikali yake.
“kila muumini ajiombee yeye mwenyewe, Familia yake,
Jamaa inayomzunguka, Nchi na Serikali inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan ili kila kitu kikiwa kimenyooka vizuri uchaguzi huo utakuwa wa amani na salama”,
amesema
Aidha amesema waendelee kuombea Upendo, Mshikamano,
Ushiriano na Umoja wa Kitaifa.
Akiongelea Eid Ul Adha amesema ni siku za Mfungo zinazofungwa
kwa siku kumi hasa kwa namba Shufaa zinazoanzia 2,4,6, 8 siku ya 10 ndiyo shufa
yenyewe na zote zinazogawanyika ambapo pia ni suna kufunga tarehe 9.