BANDA MEDIA BLOG

JAMII YATAKIWA KUWATHAMINI WATU WENYE ULEMAVU KAMA ILIVYO KWA MAKUNDI MENGINE

 

NA JOHN BANDA, DODOMA

JAMII inapaswa kulithamini na kulichulia kundi la watu wenye ulemavu kwa uzito sawa na makundi mengine kwani na wao wana haki ya kuishi, kushirikishwa na kushiriki katika hatua zote za kimaendeleo, kiuchumi, kiburudani, kimichezo, kiuongozi na hata kisiasa, hivyo lisiachwe likakata tamaa, mwishowe likageuka kuwa Tegemezi (MZIGO).

Hapa Yupo Kombo Jumbe Mohamed Maarufu, KESSY WA VISSA ambaye ajali ya gari mnamo Mwaka 2014, jijini Dar es laam ilimsababishia ulemavu wa miguu yote Miwili kwani ilikatika kabisa.

Kessy wa Vissa kabla ya Ajali hiyo iliyomsababishia ulemavu huo alikuwa anajishughulisha na Shughuli mbalimbali za kumuingizia kipato Pamoja na hivyo alikuwa anashiriki kwa ukamilifu Sanaa ya mapigano karate Shotokan.

Wavissa ambaye kwa sasa anaishi jijini Dodoma pamoja na changamoto ya ulemavu aliyonayo kutokana na kupata ajali hiyo mbaya ya gari iliyogarimu miguu yake yote miwili hakukata tamaa, bado anakimbia riadha kilomita kumi, 10 kwa kutumia Baiskel ya mikono (wheelchair).

Akingea kwa uchungu mwingi, amesema kuwa changamoto anayokumbana nayo kutoka kwa waandaji wa Marathon alizowahi kushiriki, ni kile kinachoonekana kutolitambua kundi hilo la watu walemavu na kulitengea bajeti ya zawadi kwa washindi kama ilivyo kwa makundi mengine ya watu wenye umri mkubwa, vijana na hata Watoto ambao huibuka na zawadi lakini walemavu wanageuziwa kisogo.

“Waandaji wanashindwa kutambua mchango wetu ndiyo maana wanashindwa kututengea zawadi kama ilivyo kwa wenzetu wengine, mfano  marathoni ya mwisho iliyofanyika hapa Dodoma, Pamoja na waziri mkuu kuwaelekeza waandaaji kutoa zawadi kwa kundi maalumu la wenye ulemavu lakini nilipoenda kuwaona hawakunipokea vizuri, wakanijibu kwa mkato, kuwa hakuna fungu Hilo”, amesema

Aidha anasema kutokana na kushiriki na kumaliza km.10 kwenye Marathon zilizoandaliwa na CRDB, NBC ambayo ameshiriki mara 2, BUNGE, MSOGA na TULIA Marathon ameambulia kukutana na kufahamiana na viongozi wakubwa kwa wadogo wa serikali ambao wamemtia moyo sana.

Hata hivyo anawashauri watu wa kundi hilo la watu wenye ulemavu kutobweteka wala kukata tamaa wanapokumbana na changamoto za kutengwa au kutoshirikishwa kwenye mambo ya kijamii, kwani ipo siku mambo yatajipa maana anaamini jambo la muhimu ni kutengeneza Conection kwanza huku akitiwa moyo na viongozi mbalimbali kuendelea kulipigia chapuo kundi hilo kwenye majukwaa mbalimbali.

“Ni miaka kumi sasa! Ukiachana na maneno ya faraja ninayokutana nayo lakini tambua kuwa ULEMAVU NI JANGA. jamii zetu hazijui chochote kuhusu watu wenye ulemavu ndio maana ukishakua mlemavu huwezi kuaminika japo kwa upande wangu naamini ipo siku mambo yataenda sawa”, anasema na kuongeza

Pia Kessy wa Vissa anaishukuru familia yake hasa mke wake ambaye ameendelea Kumuunga Mkono wakati wote hata baada ya kupata ajali hiyo iliyomgalimu Miguu yote miwili.

Hivi karibuni Katibu mkuu wa shirikisho la watu wenye ulemavu mkoa wa Dodoma mchungaji, Kenneth Mwilawi aliiasa  jamii ya Watanzania kuendelea kutoa ushirikiano kwa watu wenye ulemavu ambao kwa namna moja ama nyingine wameweza kuanzisha na kushiriki katika fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

Watu wenye ulemavu wamekuwa wakiijingiza katika fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi ambapo wamekuwa wakijipatia kipato chao cha kila siku hivyo ipo haja kwa jamii, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali, makapuni na watu binafsi, kuendelea kutoa mchango kwa kuliunga mkono kundi hilo kama viongozi mbalimbali wanavyosisitiza katika majukwaa.


Aidha ameongeza kuwa taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi wanaweza kuanzisha vituo, kwa ajili ya kutoa fursa mbalimbali ikiwemo elimu na mafunzo maalum kwa ajili ya kundi hilo ili watu wenye ulemavu nao wawe sehemu ya jamii inayopata fursa kama ilivyo kwa makundi mengine badala ya kuwaacha wakijitaabikia bila kujaliwa na yoyote.

SERA YA TAIFA YA MAENDELEO NA HUDUMA KWA WATU WENYE ULEMAVU

(e) Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu katika jamii (Community Based Rehabilitation – CBR). Utaratibu unaoshirikisha jamii katika utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu. Jamii katika sera hii ina maana ya familia, Serikali ya Kijiji au Mtaa au kikundi chenye malengo na mahitaji yanayolingana.

(g) Haki na fursa sawa kwa watu wenye ulemavu (equalization of opportunities for persons with disabilities). Upatikanaji wa haki, huduma na fursa sawa kwa watu wenye ulemavu sawa na wasio na ulemavu.

 




Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG