..........................................
NA JON BANDA,DODOMA
KAMPUNI ya Mtandao wa simu ya Vodacom Tanzania LTD kwa kushirikiana na Taasisi ya AfyaCheck wanamuezi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutoa huduma za Afya Bure katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma huku wakiwa na malengo ya kuwahudumia watu Elfu tano katika mikoa mitano.
Mratibu wa Kambi za Afya za twende Butiama Africa, Dkt.
Isack Maro leo Oct 5,2024 amewaambia waandishi wa Habari jijini humo kuwa, wanachokifanya kwenye Kambi hizo ni Pamoja na
Kuwapima wagonjwa, Kuwapa dawa, Ushauri na Elimu ambapo huduma zote ni bure.
Amesema kambi
hizo za kupima Afya zilizodhaminiwa na Vodacom Foundation Tanzania, zinalenga
kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwapima na
kuwatibu wanaosumbuliwa na Shinikizo la Juu la Damu, Kisukari, Saratani ya
Kizazi na matiti kwa wanawake na Tezi Dume kwa wanaume ikiwa ni Pamoja na kuwahudumia
Watoto na watu wazima.
Aidha amesema huduma hizo zimeanza kutolewa tangu jana
oct 4 watamaliza jumapili oct 6 mwaka huu, kisha watatoa huduma kama hizo katika
mikoa ya Singida, Tabora, wilaya ya Bihalamuro Kagera na Chato mkoani Mwanza.
Mkazi wa Chang’ombe jijini Dodoma, Mzee Husein Ninga
ameipongeza AfyaCheck kwa kuja na mpango huo wa kutoa huduma za Afya hasa kwa
wazee wenye umri mkubwa kwani kwa kufanya hivyo ni kumuenzi Hayati Baba wa
Taifa kwa Vitendo.
Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere alifariki Tarehe 14,10,1999 ambapo watanzania wataungana kote Duniani
kwenye kumbukizi ya miaka 25, oct
14,mwaka huu.