BANDA MEDIA BLOG

WATENDAJI WAPELEKEENI WANANCHI ELIMU YA USAFI WA MAZINGIRA

 





NA JON BANDA,DODOMA

ILI wakazi wa Halmashari ya jiji la Dodoma waweze kuepukana na magonjwa ya Mlipuko yakiwemo matumbo ya kuhara yanayosababishwa na uchafu, Watendaji wa Kata na Mitaa wametakiwa kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutunza mazingira ikiwemo kutumia sheria ya adhabu kwa wachafuzi wa makusudi.

Afisa Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu wa Jiji la Dodoma Ally Mfinanga amejitokeza mbele ya Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari na kuwataka wahusika kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi

“nitoe maelekezo kwa watendaji wa kata, mitaa, maafisa afya na mazingira waliyopo kwenye kata na mitaa kuhakikisha wanatoka maofisini kwenda kutoa elimu kwa vitendo, mwananchi akiwa ameelimika nab ado akaendelea kuchafua mazingira apewe adhabu kama sheria za mazingira zinavyoelekeza”, amesema

Aidha Mfinanga ameongeza kuwa halmashari hiyo imeyaagiza makapuni ya uzoaji taka na kuzipeka Chidaya kuimarisha magari yao na kuwa na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kazi hiyo hasa kipindi hiki cha kuelekea msimu wa mvua.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Sabasaba, Kombo Kombo amesema kumekuwa na ucheleweshaji mkubwa wa kuzoa takataka zinazozalishwa kwa wingi kwenye dampo lililopo sokoni hapo

“niseme bila kupepesa macho Pamoja na mtu tuliyepewa na jiji, kwa ajili ya kusimamia usafi sokoni, bado changamoto inakuwa kwenye usombaji wa taka ambazo zimekuwa zikibaki hata kwa zaidi ya wiki nzima kutokana na kukosekana kwa magari ya kusombea kwa wakati hali inayosababisha wafanyabiashara kuishi kwa hofu ya maganjwa ya mlipuko”,  

Aidha amesema wanaiomba serikali kuondoa takataka kwa wakati lakini pia watengeneze mitaro ya kupitishia maji machafu.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG