BANDA MEDIA BLOG

ASKOFU LUPAA ATOA SIRI YA UZEMBE KWA WANAWAKE WASIOJUA KUWAPIKIA WAUME ZAO



Askofu wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Rift Valley John Lupaa akifafana jambo wakat alipokuwa akiifunga Warsha hiyoiliyowajumuisha washiriki 50 toka wilaya ya Manyoni Mkoani Singida 

                       ..................   

                  NA JOHN BANDA, SINGIDA

ASKOFU  wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Lift Valley John Lupaa Amefichua Athali zinazosababishwa na Ubaguzi wa Kimalezi unaofanywa na baadhi ya wazazi na walezi kwa kuwalundikia kazi wanazozani ni nzito Watoto wasiowazaa wakidhani wanawakomoa kumbe ndiyo wanawatengeneza, huku wakiwaacha Watoto waliowazaa wakiwa hawana uwezo wa kujitegemea.

Askofu Lupaa ameifichua siri hiyo wakati alipokuwa Akifunga Warsha ya pili ya mitaala ya Rasilimali CCMP, iliyoandaliwa na Ushirika wa Wamama wa Kikristo (UMAKI) wa Kanisa Anglikana Tanzania, ambapo amesema kuwa kinachowatafuna Watoto wa matajiri mpaka kujikuta hawana uwezo wa kufanya kazi za kujihudumia ni kudekezwa na wazazi wao.

Amesema siku hizi baadhi ya vijana wa kike na wakiume wanashindwa kujisimamia katika Maisha yao na wengine kushindwa hata kupika kufanya usafi wa nyumba, kwa sababu walilelewa kimayaimayai kwa wazazi ama walezi wao kuwalundikia kazi Watoto baki walioishi nao wakiwemo mabinti wa kazi.

Ametoa mfano kuwa watu wa nchi za magharibi hasa wazungu walibweteka wakisema kazi nzito wapewe wenye Ngozi nyeusi, wakati wao wakijipa kazi za kuwaongoza na kuwasimamia, baadae Weusi walijikuta ndiyo wabunifu na wavumbuzi wa mwanzo wa mambo ya maendeleo Duniani, Hvyo kumpa mtu kazi kwa lengo kumkomoa ni kumnoa.

“wazazi/walezi walidhani wanawapenda sana Watoto wao na kuwanyima kufanya kazi za usafi wao, wa nyumba, kupika wakidhani wanawapenda sana huku kazi hizo wakiwalundikia mayaya, mabinti wa kazi na Watoto wasiowahusu bila kujua kuwa ndiyo wanawatengeneza”, amesema

Aidha amesema kuwa hali hiyo imekuwa ni tatizo kwa baadhi ya wanawake ambao wamekuwa wakishindwa kuwapikia chakula hata waume zao

Akiongelea kuhusu mafunzo hayo Askofu Lupaa, amesema ametoa mwaka mmoja kwa parishi zote za Dayosisi hiyo kuhakikisha zinaweka kitega uchumi kwenye kila kanisa kwa lengo la kuzitumia Rasilimali na fursa za kiuchumi ili kujiletea maendeleo.

 Nae Afisa maendeleo wa Dayosisi ya Rift Valley, Kasisi Canon, Ezra Machasa amesema jumla ya washiriki 50, wameshiriki mafunzo hayo ndani ya siku 6 ambapo wamejifunza utambuzi wa rasilimali na jinsi ya kuzitumia ikiwemo kuzitambua fursa ambazo Mungu amewapatia ili kuzitumia kwa ajili ya kujikwamua Kaiuchumi.

“changamoto kubwa iliyopo kwenye jamii ni watu wengi kutozitambua Fursa wala Rasilimali ambazo Mungu amewapati, hata kama wanazitambua bado hawazitumii ndiyo maana mradi wa  CCMP umekuja ili kuwahamasisha kuzitambua na kuzichangamkia ili wajipatie maendeleo ndani ya kanisa”, amesema

Hata hivyo washiriki hao ndiyo watakaokuwa wawezeshaji waw engine makanisani mwao.

Katibu wa Ushirika wa Wamama wa Kanisa la Anglikana Tanzania (UMAKI) Ley Canon Dkt. Margaret Ndonde akaiongea jambo wakati wakfunga mafunzo hayo

Kwa upande wake Katibu wa Ushirika wa Wamama wa Kikristo wa Kanisa la Anglikana Tanzania (UMAKI) Lay Canon, Dkt Margaret Ndonde akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Kanisa Hilo amesema wamekuja na mradi huo mahususi wa Mchakato wa kuhamasisha maendeleo ya kanisa na jamii (CCMP) kwa lengo la kuifumbua macho jamii ya kuziona fursa na Rasilimali zilizopo.

Tunawajengea uwezo ili wao wakawafundishe wenzao makanisani, ili kanisa lenyewe liwe nuru na chumvi hatimaye liwavute wanajamii, pia tunatamani mafunzo haya yakawanufaishe wanakanisa kwanza na baadae wayapeleke katika jamii,

“kanisa liwe nuru na chumvi kwa maana ya mafunzo haya yawasaidie kwenye maendeleo ya kanisa na jamii.

Aidha amesema Mradi huo unaendelea kwenye Dayosisi 13 za kanisa angalikana hapa nchini huku malengo yakiwa ni kuzifikia Dayosisi zote 28 za kanisa hilo, “tunajivunia pia mradi mwingine wa uundwaji wa vikundi vya Akiba na mikopo unaotekelezwa kwenye Dayosisi 19 na kwamba tayari asilimia kubwa ya vikundi vilivyoundwa vimeshasajiliwa kisheria”, amesema 






Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG