BANDA MEDIA BLOG

USHINDI WA DKT, SAMIA 2025 SIYO WA PEREPETE ZA MDOMONI WALA NYIMBO ZA HIYENA HIYENA-MAKINDA

 




NA JOHN BANDA, DODOMA

KAMISAA wa Sensa Tanzania, Anna Makinda amewambia wanawake na Samia kuwa Ushindi wa Rais huyo wa Sasa kwenye uchaguzi wa Mwaka ujao hautaki Maneno Matupu unataka vitendo hasa kujiandikisha na kupiga Kura.

Akiongea kwenye Hafra ya Wanawake na Samia Gala, iliyifanyika jijini Dodoma ikiwahusisha wanawake hao Kutoka mikoa Nane Nchini Makinda amesema Ushindi kwenye uchaguzi ujao siyo wa Hiyenahiyena wala perepete za mdomoni pekee.

Kamisaa Huyo ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema ili Rais Samia Suluhu Hassan aweze kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi ujao wanawake hao wahakikishe Wanawahamasisha Wananchi  wajiandikishe na kisha kwenda kupiga Kura.

"Ni kweli Wanawake mnafanya Kazi nzuri ya Kumuunga Mkono Rais Samia kwenye Kazi anazofanya kwa ajili ya watanzania, ila kumbukeni Ushindi kwenye uchaguzi ujao si wapelepete mdomoni Tu au kuimba hiyena hiyena unataka vitendo, msibaki kuimba mkasahau kuhamasishana kupiga Kura zitakazompitisha mama 2025", amesema

Aidha Makinda amesema Rais Samia ni Rais tuliyopewa na Mungu kwani wakati akiapishwa wengi walimbeza lakini sote ni mashahidi kwa Kazi  kubwa alizofanya mpaka sasa, Kwa ajili ya Jamii ya Watanzania, hata wanaume wenyewe wanashangaa amewezaje.

Kwa upande wake Mbunge wa Dodoma mjini Anthon Peter Mavunde, amewapongeza wanawake na Samaia kwa Kazi Nzuri wanayoifanya ambapo aliwaunga mkono kwa kuwaahidi kuwanunulia Vyombo na kuwaongezea mtaji  kwa ajili ya kuanzisha mradi wa Mapishi

Naye mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amelielezea kundi hilo la wanawake na Samia kuwa limejipambanua nchi nzima kwa ajili ya kumuunga mkono na kumtia Moyo Rais Samia kwa vitendo

Amesema Miaka ya hivi karibuni wanawake walikuwa wanagombea nafasi za uongozi kwa uoga na mashaka kutokana na kutojiamini, lakini sasa wamepewa ujasiri na Rais aliye madarakani kwa uongozi wake mahili na wa kuigwa tena akiwa mwanamke.

Awali akisoma Risala mwenyekiti wa Wanawake na Samia mkoa wa Dodoma, Fatuma Mdidi amesema  Kazi ambazo wameshazifanya ni Pamoja na kuibua vitendo vya ukatili 47, walivyofanyiwa wanawake na Watoto, kuukijanisha mkoa kwa kutengeneza vyungu vya maua, ushiriki wa mbio za mwenge, kutoa elimu ya maadili, misaada mbalimbali kwa makundi yasiyojiweza Pamoja na kushiriki shughuli za kiserikali ikiwemo kuhamasisha jamii kujiandisha kwenye Daftari la mpiga kura mwaka huu.

Ameongeza kuwa walioshiriki katika hafla hiyo ni pamoja na wanawake kutoka mikoa 8, ya Tanzanzia Bara na kwamba kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2025 wanasimama na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa CCM.

















Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG