
Kwa niaba ya Baraza la Waislamu nchini Tanzania BAKWATA, Naibu Katibu mkuu wake Sheikh Mohamed Khamis amesema kuelekea mwaka 2050 ni muhimu serikali kuhakikisha kuwa inadhibiti michezo ya Kamari kutokana na namna inavyoua nguvu kazi ya jamii na kuwatia Vijana wengi kwenye umaskini wa Kipato.
Wakati wa kupitia rasimu ya kwanza ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 kwa Viongozi wa dini leo Jumatatu Jijini Dar Es salaam, Sheikh Khamis pia amependekeza kuwa ni muhimu Taifa likawekeza kwenye kujenga jamii ya watu wabunifu na wanaopenda kujifunza na kufanya kazi.
- BAKWATA pia wameshauri serikali kuruhusu mahakama ya Khazi katika jitihada za kuimarisha maadili ya Kijamii, pamoja na kutenga maeneo maalum kwaajili ya ibada kwenye Ofisi zote za Umma na zile za binafsi pamoja na kuweka bayana kuwa Familia inaundwa na Baba (Mwanaume) na Mama (mwanamke)ili kupambana na umagharibi na uvunjifu wa maadili.
Tags
HABARI