BANDA MEDIA BLOG

𝐖𝐀𝐉𝐔𝐌𝐁𝐄 𝐖𝐀𝐏𝐈𝐓𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐀𝐙𝐈𝐌𝐈𝐎 𝐋𝐀 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐏𝐈𝐓𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐍𝐀 𝐃𝐊𝐓. 𝐌𝐖𝐈𝐍𝐘𝐈 𝐊𝐔𝐆𝐎𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐍𝐀𝐅𝐀𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 & 𝐙𝐀𝐍𝐙𝐈𝐁𝐀𝐑

 

𝑾𝒂𝒋𝒖𝒎𝒃𝒆 𝒘𝒂𝒎𝒆𝒇𝒂𝒏𝒚𝒂 𝒎𝒂𝒂𝒎𝒖𝒛𝒊 𝒉𝒂𝒚𝒐 𝒌𝒘𝒂 𝒌𝒖𝒛𝒊𝒏𝒈𝒂𝒕𝒊𝒂 𝑲𝒂𝒕𝒊𝒃𝒂 𝒚𝒂 𝑪𝑪𝑴 𝒊𝒃𝒂𝒓𝒂 𝒚𝒂 100 𝒌𝒊𝒇𝒖𝒏𝒈𝒖 𝒌𝒊𝒅𝒐𝒈𝒐 𝒄𝒉𝒂 2 𝒊𝒏𝒂𝒚𝒐𝒆𝒍𝒆𝒛𝒂 𝒌𝒖𝒘𝒂 𝑴𝒌𝒖𝒕𝒂𝒏𝒐 𝑴𝒌𝒖𝒖 𝒏𝒅𝒊𝒐 𝒌𝒊𝒌𝒂𝒐 𝒌𝒊𝒌𝒖𝒖 𝒄𝒉𝒂 𝑪𝑪𝑴 𝒄𝒉𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒎𝒂𝒎𝒍𝒂𝒌𝒂 𝒚𝒂 𝒎𝒘𝒊𝒔𝒉𝒐

 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameridhia kwa kauli moja kuwapitisha Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, kuwania tena nafasi hizo katika uchaguzi wa mwaka huu 2025.

 Hayo yametokana na mapendekezo waliyoyatoa wakati wa michango yao baada ya kutazama na kusikiliza utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Hivyo, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imeketi na kuandaa Azimio hilo na kuwasilishwa kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu katika ukumbi wa JKCC Jijini Dodoma leo tarehe 19 Januari, 2025 ambapo kwa pamoja wameridhia kwa asilimia 100.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG