Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla ameeleza mbele ya vyombo vya habari jijini Dodoma, utaratibu wa kupatikana kwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara atakayemrithi Komredi Abdulrahman Kinana ambaye aliamua kuuachia wadhifa huo
Amesema kuwa jina la mrithi huyo litapatikana baada ya kupendekezwa na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM na kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu utakaofanyika Januari 18 na 19 mwaka huu, ambapo wajumbe watapata fursa ya kupiga kura ya ndiyo au hapana.
Wandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwajibika katika mkutano kati yao na SPA Makalla ambaye ni Katibu wa Itikadi, Uenezi na mafunzo wa Chama cha Mapinduzi
Tags
SIASA
