BANDA MEDIA BLOG

Makomandoo wa UK wafichua: Kikosi maalumu kilipewa 'kibali cha dhahabu' cha kuulia raia Afghanistan

 

  • Makomandoo wa UK wafichua: Kikosi maalumu kilipewa 'kibali cha dhahabu' cha kuulia raia Afghanistan

Askari wa zamani wa jeshi la Uingereza ameiambia tume ya uchunguzi kuwa makomandoo wa kikosi maalumu cha nchi hiyo walikuwa na sera waliyowekewa ya kuua raia bila kujali wakati wa mashambulizi waliyokuwa wakifanya dhidi ya Taliban nchini Afghanistan.

Ushahidi huo uliotolewa na idadi ya wanajeshi na makamanda saba ni sehemu ya uchunguzi wa mwenendo wa kikosi maalumu cha Uingereza, kikiwemo cha SAS, katika jimbo la Helmand, nchini Afghanistan kuanzia mwaka 2010 hadi 2013.
 
Askari huyo aliyetambulishwa kwa anuani ya N1799 amesema: "wakati wa operesheni hizi ilikuwa ikisemwa, 'wanaume wote wenye umri wa kuweza kupigana wauliwe' kwa kulengwa, bila kujali kama ni tishio; na hii ni pamoja na hata wale wasio na silaha".
 
Kwa mujibu wa N1799, "katika kisa kimoja ilitangazwa kwamba mto wa kulalia uliwekwa juu ya kichwa cha mtu kabla ya kuuliwa kwa bastola" na akaongeza kuwa, yeye binafsi alishtushwa na umri wa wahanga na mbinu zilizotumiwa kuwaulia Waafghani.
 
Shahidi mwingine ambaye ni komandoo wa zamani wa jeshi la Uingereza ameiambia tume ya uchunguzi kama alivyonukuliwa na shirika la utangazaji la nchi hiyo BBC kuwa, kikosi hicho maalumu kilikuwa na alichokiita "kibali cha dhahabu cha kuwavua na hatia ya mauaji".
 
Kwa mujibu wa ushuhuda ulioripotiwa na gazeti la New York Times, askari mmoja aliuliza katika barua pepe kama vitengo vya SAS vilikuwa vinajitengenezea matukio na mazingira ya kuwaruhusu kuwaua wapiganaji wa Afghanistan na akajibiwa na afisa mwingine kwamba, "Waafghani hawa ni wajinga sana wanastahili kufa."
 
Wanajeshi wa Uingereza na wa vikosi vingine vya Magharibi waliondoka nchini Afghanistan mwaka 2021, kufuatia miongo miwili ya uasi ulioendeshwa dhidi yao na kundi la Taliban.
Kwa mujibu wa ripoti rasmi, Uingereza ilipoteza wanajeshi 457 wakati iliposhiriki katika kuikalia kwa mabavu nchi hiyo.../

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG