Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akipokea taarifa ya utekelezaji wa Miundombinu ya Mawasiliano katika Nyanda za juu Kusini kutoka kwa wataalamu wa taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika kikao kilichofanyika tarehe 11 Januari, 2025 katika Ofisi za TCRA zilizopo mkoani Mbeya.
Katika kikao hicho wataalamu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) waliwasilisha taarifa za utekelezaji ikiwemo hali ya upatikanaji wa Mawasiliano, Ujenzi wa Miundombinu ya Mawasiliano pamoja na Ujenzi wa Minara ya Mawasiliano.



