BANDA MEDIA BLOG

DC MUHEZA ACHANGIA PIKIPIKI 10 UVCCM MKOA WA TANGA



Mkuu wa Wilaya ya Muheza - Mhe Zainab Abdallah, jana kwenye Kongamano la UVCCM wilaya ya Muheza ameunga mkono juhudi za UVCCM kwa kuchangia vifaa vya ujenzi wa jengo la katibu wa UVCCM wilaya ya Muheza pamoja na 5,000,000/= fedha taslim kwa ajili ya gharama za ufundi ili kuhakikisha nyumba hiyo inakamilika kwa wakati na kutoa fursa kwa mtendaji wa UVCCM kufanya kazi katika mazingira bora.

Aidha, amenukuliwa akisema; “Nimefanya kazi Mkoa wa Tanga kwa miaka 7, mimi ni zao la UVCCM; nina wajibu wa kuacha alama ya kudumu katika Mkoa huu. Hivyo kwa mapenzi makubwa nachangia pikipiki 10 kwa wilaya zote za Mkoa wa Tanga zikawasaidie watendaji wa jumuiya yetu. Pikipiki hizi pamoja na majukumu mengine zikatumike kwenda kuskiliza na kutatua kero za vijana, zikatumike kusemea kazi nzuri zinazo fanywa na Mwenyekiti wetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Dr Samia Suluhu Hassan





 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG