BANDA MEDIA BLOG

SIMBACHEWENE ASHIRIKI IBADA YAKUMBUKIZI YA HAYATI EDWADI LOWASA MONDULI

 

Waziri simbachawene ashiriki ibada ya kumbukizi ya hayati Edwadi Luwasa monduli 

............

Na Barnabas Kisengi Monduli Arusha

February 09. 2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameungana na wanafamilia, viongozi wa chama, serikali na wananchi katika Ibada ya shukrani ya Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa, iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Monduli mkoani Arusha, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Taifa lilipompoteza kiongozi huyo.

Akizungumza kwa niaba ya Familia ya Hayati Edward Lowassa, Mwanae  ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wote waliokuwa pamoja tangu Baba yao alipofariki hadi hivi sasa huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa wa kuwa pamoja na familia hiyo tangu Baba yao alipoanza kuugua hadi umauti ulipomkuta 

"Kwa unyenyekevu mkubwa ninawaomba Watanzania wote tuendelee kumuenzi Hayati Edward Lowassa kwa yale yote mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake" amesisitiza Fredrick Lowassa

Naye, Baba Askofu Mstaafu  wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dkt. Solomon Masangwa ameitaka familia hiyo kuzidi kumuangukia Mwenyezi Mungu katika kila jambo wanalolifanya.

Mwisho.





Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG