BANDA MEDIA BLOG

ALIYEFANYA UPEDESHEE WA KUMWAGA PESA KWENYE HARUSI YAKE AFUNGWA JELA



 Mpambaji maarufu kutoka jimbo la Kano, Abdullahi Musa Huseini, anayejulikana kwa jina la mtandaoni “Amuscap,” amehukumiwa kifungo cha miezi sita na Mahakama ya Juu katika jimbo la Kano kwa kosa la kumwaga noti za Naira katika harusi yake.

Hussein alikiri shtaka moja la matumizi mabaya ya Naira mbele ya Hakimu S.M Shuaibu wa Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa taarifa ya EFCC iliyotolewa katika mtandao wa X, bwana harusi alikamatwa katika sherehe ya harusi yake Disemba mwaka jana kufuatia “taarifa za kiintelijensia.”

“Mshatakiwa alikamatwa katika harusi yake kufuatia taarifa za kuaminika za matumizi mabaya ya fedha ya Nigeria,” imesema EFCC.

Wakala wa kupambana na ufisadi imesema kwamba Huseini alikamatwa “akicheza mziki huku akimwaga fedha zinazofikia kiasi cha Naira 100,000 katika noti za elfu moja moja zilizotolewa na Benki Kuu ya Nigeria.

Kushusha thamani fedha za nchi hiyo kwa kuzimwaga, ni utamaduni uliozoeleka katika sherehe za Nigeria kama alama ya utajiri na furaha, lakini ni kosa chini ya kifungu cha 21(1) cha Benki Kuu, 2007.”

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG