BANDA MEDIA BLOG

Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

 


Na. Leah Mabalwe, Dodoma

SHULE ya Sekondari Nala imefanikiwa kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kutokana na utekelezaji wa dhamira ya serikali ya awamu ya sita wa kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma ya chakula na lishe shuleni.


Kauli hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Nala, Joseph Chambo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliotembelea shule yake kujiona utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni hapo, katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya Sita.


“Katika utekelezaji wa Muongozo wa kitaifa wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi umetunufaisha sana. Hapo awali kulikuwa na mahudhurio hafifu sana shuleni kwetu. Pia hata tukiwa darasani wanafunzi walikuwa na uelewa wa chini na hata ufaulu ulikuwa sio mzuri sana,

lakini Kufuatia utelekezaji wa mwongozo huu shule yetu sasa imekuwa ni ya mfano. Watoto wanahamasika kuja shule na hata ufaulu umepanda kwa kiasi kikubwa kulinganisha na hapo awali. Sisi kama walimu tumetekeleza muongozo huo kwa kiasi kikubwa sana’’ amesema 


Vilevile, aliongeza kuwa utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni hapo ulisaidia kuepusha vishawishi kwa wanafunzi hasa wanafunzi wa kike. “Huduma ya chakula na lishe imesaidia kuchochea wanafunzi kuja shuleni na kusoma kwa amani na utulivu huku wakifuatilia vipindi kwa umakini, jambo lililopelekea kupanda kwa kiwango cha ufaulu” alisema Mwl. Chambo.


Nae, Mwanafunzi Vanessa Fidelis aliishukuru serikali kwa utaratibu wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni hapo.

“Naishukuru sana serikali kwa kuleta huduma hii shuleni kwasababu imesaidia kuhamasisha wananfunzi kupunguza utoro na imesaidia kusoma kwa muda mrefu hasa vipindi vya jioni. Utaratibu huu umesaidia kukuza taaluma yetu na kupandisha kiwango cha ufaulu” alisema Fidelis.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG