Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania UWT Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) ahudhuria Dua Maalum ya kuwaombea Viongozi wa Kitaifa, Kuliombea Taifa liendelee kuwa na Amani, Sambamba na kuwaombea Mufti wa Tanzania na Mashekh waliotangulia Mbele za Haki.Katika Dua hiyo Makamu Mwenyekiti aliambatana na Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT, iliyofanyka kwenye Viwanja vya Msikiti wa Mohammed VI, Kindondoni Jijini DSM, Makamu Mwenyekiti amesema ni Vyema Watanzania kumrudia Mwenyezi Mungu na Kumuomba kheri ili Azidi, kutubariki na kutulinda na Maasi ambayo ndiyo chanzo Cha kuvurugika kwa Amani ambayo ni Tunu kubwa iliyoundwa na kutunzwa na Viongozi Wetu wa Kitaifa.
Akiwa Mgeni Rasmi kwenye Dua hiyo Waziri Mkuu wa Tanzania Mh, Kassim Majaliwa Amewasihi Watanzania kuilinda Amani ya Nchi hususani katika kipindi hiki Cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, huku akiwahakikishia Serikali haitomvumilia Mtu yeyote atakaejaribu kuivuruga Amani ya Nchi kwa Kufanya Matendo yasiyofaa kwenye jamii.
Tags
DINI NA MADHEHEBU


