.........................................
Na Mwandishi Wetu, Pemba
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka
Viongozi na wanachama wake kisiwani pemba kujiandaa kisaikolojia na kujipanga kimkakati
tayari kushiriki uchguzi
mkuu wa oktoba mwaka huu
Pia
chama hicho kimesema Uchaguzi
si jambo dogo bali ni mapambano ya
sera na hoja si kama kucheza
lelelmama au singeli.
Maelezo
hayo yametolewa na Katibu wa
Kamati Maalum ya NEC
Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto
Khamis , alipozumgumza na makundi
ya vijana Wahamasishaji na Wasanii katika Ukumbi wa Makonyo huko Wawi Kisiwani hapa.
Mbeto alisema kila kiongozi na Mwanachama kwa nafasi zao, wanatakiwa
kuhahakikisha wanafanya kila linalowezekana
ili kupata ushindi wa kidemokrasia kwa kuwahamasisha wanachama na
wananchi.
Alisema
matokeo ya ushindi wa
uchaguzi ni baada ya chama kutangaza sera zake ,wananchi
kupiga kura ,kuhesabiwa na matokeo kutangazwa.
Alisema ni matarajio ya kila chama cha
siasa kipate idadi kubwa ya kura
,kwakuwa wala Uchaguzi si
simulizi za hadithi au maneno matupu.
Chama chenu kinawataka viongozi wote
mjipange na kujiandaa kimkakati
kuelekea Oktoba Mwaka huu. Uchaguzi umeshapiga hodi hivyo lazima
tukumbushane mapema na kuanza kujipanga "Alisema Mbeto.
Aidha ,alisem pamoja na kila
unapomalizika uchaguzi mkuu mmoja ,
CCM hujiandaa kwa uchaguzi mwingine,
aliwataka wanachama kutobweteka na kufanya mambo kwa mazoea.
"Uchaguzi hubadilika kulingana na mazingira
husika.Hata Malaria ukipima utakuta
idadi ya juu au ya chini ya wadudu wake.Uzoefu katika kila uchaguzi una
uzoefu na mazingira yake "Alisema
Mbeto
Hivyo basi, Katibu huyo Mwenezi
alisema hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi peke yake bila kuwashirikisha
wenzake huku akiwataka viongozi wa
CCM kushirikiana na wanachama wao.
"Wasanii jiandaeni kutunga mashairi ya nyimbo nzuri za hamasa na kampeni .Wahamasishaji lazima mpite kila nyumba, kiambo kwa kiambo,shehia hadi shehia kuomba kura kwakuwa huo ni wajibu wa kidemokrasia "Alieleza
Alisema
nyimbo zote zitakazotungwa zitahakikiwa
mapema na kupasishwa kabla ya kuimbwa , hivyo aliwataka watunzi wa
nyimbo hizo kuanza kutunga mashairi yatakayovutia na kuelimisha wananchi kuhusu uchaguzi mkuu.
